Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji (Rufaa) Mhe. Jacobs Mwambegele (kulia) akiongoza Kikao cha Tume kilichokutana leo Agosti 17,2023 jijini Dodoma. Pamoja nae ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mhe.Mbarouk Salim Mbarouk.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika kikao kilichokutana leo Agosti 17,2023 Jijini Dodoma.
***************
Na Mwandishi wetu, Dodoma.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa vibali
vya kutoa Elimu ya Mpiga Kura katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali
na Kata sita za Tanzania Bara kwa asasi tatu za kiraia.
Taarifa ya Tume iliyosainiwa na
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima
imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya Tume kukutana katika kikao chake leo
Agosti 17,2023 jijini Dodoma.
“Tume imefikia uamuzi huo kwa
kuzingatia kifungu cha 4C cha sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 na kanuni
ya 3 ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka
2020, inayoipa Tume jukumu la kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima, kuratibu na
kusimamia taasisi na asasi za kiraia zinazotoa elimu hiyo,” ilisema sehemu ya
taarifa hiyo.
Kailima amezitaja asasi za kiraia
zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura na maeneo watakayotoa elimu
hiyo kuwa ni Alpha and Omega Reconciliation and Peace Building (AREPEB), itakayotoa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya
Mbarali katika Jimbo la Mbarali, Umbrella of Women and Disabled Organisation
(UWODO) itakayotoa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Madaba katika Kata ya
Mtyangimbole na Bright Child Development Tanzania (BRIGHT CHILD), Halmashauri
ya Wilaya ya Misungwi katika Kata ya Mwaniko.
Aidha, Tume imetoa kibali cha utazamaji
kwa Asasi ya kiraia ya Bridge Development Trust Organization (BRIDETO) ambayo
iliomba kutazama uchaguzi mdogo katika Kata ya Mwaniko iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Misungwi na Kata ya Nala katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Kailima amesema katika taarifa hiyo
kuwa, Tume imefikia uamuzi huo wa kutoa kibali hicho kwa kuzingatia kanuni ya
16(5) ya Kanuni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za
mwaka 2020
Amesema katika utekelezaji wa jukumu la
kutoa elimu ya mpiga kura, asasi hizo zitapaswa kuzingatia Mwongozo wa Elimu ya
Mpiga Kura wa Mwaka 2020 katika kipindi chote cha kutoa elimu hiyo katika
uchaguzi mdogo.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi mdogo
iliyotolewa na Tume, uteuzi wa wagombea katika uchaguzi huo utafanyika Agosti 19,
2023 na Agosti 20 hadi Septemba 18, 2023 kitakuwa ni kipindi cha kampeni kwa
vyama vya siasa na wagombea, na Jumanne ya Septemba 19, 2023 itakuwa ni siku ya
uchaguzi.
“Tume inatumia fursa hii
kuzipongeza asasi zote za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga
kura na utazamaji wa uchaguzi, na inazikumbusha asasi hizo kuzingatia sheria,
kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo ya Tume katika kipindi chote cha
utekelezaji wa majukumu yao. ”
alisema Kailima katika taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Tume vibali hicho kitatumika
kuanzia tarehe Agosti 18, 2023 hadi Septemba 18, 2023.