Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 16 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Mendeleo ya Jamii Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) leo tarehe 16 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo Bi. Aziza Kheir.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba akifafanua jambo kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, tarehe 16 Agosti, 2023, jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Ali Omar King akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Neema Mwandabila akichangia jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) leo tarehe 16 Agosti, 2023 Bungeni jijini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, tarehe 16 Agosti, 2023, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (wa nne kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Katundu (wa tano kutoka kuhoto), Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba (wa nne kutoka kulia) na baadhi ya watendaji wa mfuko huo mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo kwa mwaka 2022/23 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni tarehe 16 Agosti, 2023, jijini Dodoma.
……….
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhishwa na jitihada za serikali chini ya uongozi wa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Pongezi hizo zimetolewa Agosti 16, 2023 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq kwenye kikao cha kamati cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo kwa mwaka 2022/23.
Mhe. Toufiq amesema miongoni mwa jitihada hizo ni kuanza kulipa deni la michango ya kabla ya mwaka 1999 ambapo hadi sasa kiasi cha Sh.Trilioni 2.17 kimelipwa kati ya Sh.Trilioni 4.6.
Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, amesema hali ya kifedha kwenye mfuko imeendelea kuimarika kufuatia uamuzi huo wa serikali kwa kulipa michango ya wanachama wa uliokuwa Mfuko wa PSPF kabla ya mwaka 1999.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Riziki Lulida pamoja na Mjumbe wa kamati, Mhe. Neema Mwandabila, wamepongeza mfuko kwa matumizi ya Tehama kwenye utoaji huduma kwa wanachama huku wakishauri iendelee kujiimarisha kidigitali ili kusomana na mifumo mingine.
Akijibu hoja za wajumbe, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba, amesema uhai wa mfuko ni endelevu kwa mujibu wa tathmini iliyofanyikia mwaka 2020 na unatarajiwa kufanyiwa tathmini nyingine mwaka huu.