Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya Arusha Lutheran Medical Center ALMC Godwel Kivuyo akiongea na waandishi wa Habari kuelezea Maendeleo ya upasuaji wa Nyonga na magoti unaofanywa na timu ya madaktari wanotembea Kutoka Marekani mapema Leo Jijini Arusha
Dkt.bingwa Dkt.Steven Meyer Kutoka Taasisi ya mifupa STEMM akiongea na waandishi wa Habari kuelezea Maendeleo ya upasuaji wa Nyonga na magoti unaofanywa na timu ya madaktari wanotembea Operation Walk Kutoka Marekani mapema Leo Jijini Arusha ambapo hadi Leo wagonjwa 35 wameshafanyiwa upasuaji.
Mratibu wa zoezi hilo la Mpango wa Rais Samia Lazaro Nyalandu akiongea na waandishi wa Habari kuelezea Maendeleo ya upasuaji wa Nyonga na magoti unaofanywa na timu ya madaktari wanotembea Operation Walk Kutoka Marekani mapema Leo Jijini Arusha ambapo hadi Leo wagonjwa 35 wameshafanyiwa upasuaji.
…………..
Na Ahmed Mahmoud
Shirika la Upasuaji unaotembea (Operation Walk) limepanga kufanya makubaliano maalumu na Serikali Kwa ajili ya kuongeza wingi wa Timu zinazokuja kufanya huduma za matibabu na upasuaji Kwa Kanda mbalimbali hapa nchini.
Aidha Mpango wa Upendo wa Mama Samia (Samia Love) utatangaza muda sio mrefu ujio wa madaktari bingwa wanawake ambao wamevutiwa kwanza na Rais Dkt.Samia kama Rais pekee Mwanamke Afrika lakini wamevutika na ugeni huu ulivyopekelewa nchini
Akiongea na vyombo vya Habari Mkurugenzi Mtendaji wa hospital ya Arusha Lutheran Medical Center ALMC Godwel Kivuyo Amesema kuwa wimbi Hilo limepelekea idadi kubwa ya wahitaji kukosa nafasi hiyo ya matibabu ya upasuaji wa Nyonga na magoti.
Alisema wamekuwa wakishirikiana nao kufanya upasuaji ambao umeenda vizuri Pamoja na madaktari wa kitanzania wakitoa msaada kwenye huduma za Dawa za usingizi wauguzi na madaktari hao kupata uzoefu na mafunzo Kwa kushirikiana uzoefu wa Teknolojia mpya Kwa pande zote.
Kwa Upande Wake Dkt.bingwa Dkt.Steven Meyer Kutoka Taasisi ya mifupa STEMM ameendelea kusema moyo ule ule alionyesha Rais Samia Suluhu Hassan kutaka huduma za matibabu ya kibingwa Kwa Watanzania ndio utaendelea kuwavuta kuja nchini kipindi kingine ili Kutoa huduma hizo.
Alisema wameendelea na huduma hizo za upasuaji na siku zote wametoka usiku na kuanza Kazi mapema kuanzia Alfajiri Kwa kufanya Kazi bega Kwa bega na wauguzi na madaktari wa kitanzania wakibadilishana sio tu uzoefu lakini tukibadilishana mbinu husika za upasuaji na teknolojia mpya ambazo zinaendelea kubuniwa kila wakati.
Hata hivyo Mratibu wa zoezi hilo la Upendo wa Rais Samia Lazaro Nyalandu Amesema Muda sio mrefu watapokea madaktari bingwa wanawake ambao wameonyesha kuja kumuunga mkono Rais Mwanamke Afrika sanjari na mapokezi ya madaktari wenzao wa magoti na Nyonga walivyopokelewa kwa ukarimu ndio vimewavuta kuja nchini na dhamira yao ni kwenda maeneo yote ya nchi Kutoa huduma za matibabu .
Amesema kwamba wataendelea na dhamira hiyo Kwa madaktari wa hapa nchini na nje kufanya kliniki Kwa pamoja kwenye kila pembe ya nchi kuhakikisha Watanzania wanapata huduma Bora za matibabu ya kibingwa hususani ya Nyonga na magoti sanjari na magonjwa mengine.
“Mpango huo wa Mama Samia Love una lengo la kuwagusa wananchi sio Kwa ukanda huu wa kaskazini Kwa kuangalia na Kanda nyinginezo nchini Kwa kuona ni jinsi Gani madaktari wa Ndani na nje wanaweza kushirikiana mazoezi kuokoa maisha ya watu katika majanga na mitihani inayotupata sisi wote Kwa nyakati tofautihasa wakati mtu anauhitaji kutembea asimame alishe familia yake ajenge Taifa lake”