Mkurugezi wa Mgahawa wa Ustadhi Food Restaurant Bi. Radhia Awadhi Daffa ametoa msaada wa mahitaji muhimu wenye thamani ya Shilingi milioni moja kwa wanafunzi wasioona katika Shule ya Msingi Same,Mkoani Kilimanjaro kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika program ya ‘Tabasam na Mama’
Bi Radhia amesema ametoa msaada huo kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa anaguswa na matatizo mbalimbali ya watoto wenye uhitaji hapa nchini kwa kuwachangia gharama za matibabu na kuwapatia misaada mbalimbali.
“Ustaadhi Food Restaurant tumeamua kuendeleza program ya Tabasam na Mama kwa kuchangia mahitaji muhimu kwa wenye uhitaji na program hii kwetu itakuwa endelevu”amesema Bi.Radhia
Mbali na hayo pia ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same na Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kuwafikia watu wenye uhitaji.
Aidha Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wakina mama kuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya.
Mkuu wa shule ya Msinzgi Same Elimu ya Awali Hurumar Mgonja amemshukuru Bi Radhia Awadhi kwa msaada aliotoa kwa watoto hao na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano kwa kuwasaidia watoto wenye uhitaji.