KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mzee Ramadhani Nyamka akipokea ripoti kuhusu Afya ya Akili Magerezani leo Agosti 14, 2023 katika Ofisi ndogo ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo iliyopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Ripoti hiyo imekabidhiwa kwake na Profesa Joseph Mbatia ambaye ni Kiongozi wa utafiti huo uliofanywa na Asasi ya Afya ya Akili Tanzania (MEHATA) kwa kushirikiana na Wataalam wa Jeshi la Magereza. Ripoti hiyo imeandaliwa kwa Lugha ya Kiswahili ili kuwajengea jamii na watumiaji urahisi wa kuielewa Ripoti hiyo.
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, Mzee Ramadhani Nyamka(wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Profesa Joseph Mbatia(wa pili kutoka kushoto) ambaye ni Mtafiti pamoja na baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Magereza walioshiriki katika tukio hilo la uwasilishaji wa Ripoti kuhusu Afya ya Akili Magerezani leo Jijini DSM. Wa Pili kutoka kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Dar es Salaam, ACP. George Wambura na Kulia ni Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga, ACP. Dkt. Juma Mwaibako. Picha zote na Jeshi la Magereza.