Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi maalumu, Mhe.Dorothy Gwajima akiambatana na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma wameshuhudia mchezo kati ya Simba na Yanga na kushiriki zoezi la ugawaji wa Medali pamoja na kukabidhi Ngao ya jamii kwa Timu ya Simba SC, baada ya kuibuka mshindi kwa kuishinda Yanga SC mikwaju ya penati 3-1 baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya 0-0.
Mechi hiyo imechezwa leo Agosti 13 2023 uwanja wa Mkwakwani Tanga.