Mkurugenzi wa EPZA Charles Itembe akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea mkoan i Ruvuma ambao wanatarajiwa kulipwa fedha za fidia ya ardhi.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwengemshinndo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakiwa kwenye mkutano wa hadhara na Mkurugenzi wa EPZA ,Serikali imetoa shilingi bilioni 5.3 kwa ajili ya fidia ya ardhi kwa watu 900
Na Albano Midelo,Songea
Serikali ya Awamu ya Sita imetenga shilingi bilioni 5.3 ili kuanza kuwalipa wananchi 900 fidia ya ardhi ya eneo la Export Processing Zone Authority (EPZA) lenye ukubwa wa zaidi ya hekta 5000 katika kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa EPZA Charles Itembe kwenye Mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mwengemshindo uliofanyika hivi karibuni kwa lengo la kufanya uhakiki wa wananchi watakaonufaika na fidia hiyo ili waanze kulipwa.
Mkurugenzi huyo wa EPZA amewahakikishia wananchi hao kuwa madai yao yamefikia hatua ya ukamilishaji wa malipo ili wananchi waanze kulipwa na serikali ianze kuliendeleza eneo hilo baada ya wananchi wote kulipwa fidia.
Hata hivyo Itembe alisema malipo hayo kwa mara ya kwanza yalilipwa kwa baadhi ya wananchi na awamu ya pili yatatolewa kwa wananchi ambao hawakulipwa.
Hata hivyo Itembe alisema malipo hayo kwa mara ya kwanza yalilipwa kwa baadhi ya wananchi na awamu ya pili yatatolewa kwa wananchi ambao hawakulipwa.
Amesisitiza kuwa kabla ya kuanza kulipwa utafanyika uhakiki wa majina katika ofisi ya kata Mwengemshindo ambapo wanufaika watahakikiwa kwa kuleta viambatanisho vikiwemo kitambulisho, picha, pamoja na barua kutoka Serikali ya Mitaa ili malipo yalipwe kwa mtu anayestahili na kwamba malipo yote yatalipwa kwa kupitia Akaunti za benki.
Mkurugenzi huyo wa EPZA amesema Serikali baada ya kukamilisha malipo hayo na kupewa hatimiliki ya eneo hilo itaanza uwekezaji kiuchumi hivyo kuchochea uchumi wa mji wa Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Naye katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba akizungumza kwenye mkutano huo amewataka wananchi wa Kata ya MwengeMshindo kujitokeza kwenye zoezi la Uhakiki ili kuondoa malalamiko yanayoweza kuathiri zoezi hilo.

“EPZA wamekuja kulipa fidia ya viwanja na kila mwananchi mnufaika wa fidia hizi atalipwa kulingana na ukubwa wa eneo lake, na kila mnufaika atalipwa fidia kulingana na uthamini uliofanyika bila udanganyifu wowote’’,alisisitiza.
Kwa upande wake Mthamini wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Alex Mshana aliitaja kero kubwa ya wananchi wa Mwengemshindo ilikuwa ni madai ya fidia ya ardhi eneo la EPZA Mwengemshindo ambapo sasa serikali imetoa fedha za kuwalipa.
Amesema mara baada ya malipo ya fidia hiyo wananchi watatakiwa kupisha maeneo hayo ili yaendelezwe na uwekezaji wa matumizi ya umma kupitia EPZA uweze kufanyika.
Amesema mara baada ya malipo ya fidia hiyo wananchi watatakiwa kupisha maeneo hayo ili yaendelezwe na uwekezaji wa matumizi ya umma kupitia EPZA uweze kufanyika.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi,Diwani wa Kata ya Mwengemshindo Mheshimiwa Osmond Kapinga ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha za fidia kwa wananchi hao hivyo kumaliza kero hiyo ya muda mrefu.