Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakishindana mbio katika Bonanza lililofanyika leo Agosti 12, 2023 katika Viwanja vya Gwambina Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Mbagala Mhandisi Elirehema Makacha akizungumzia Bonanza lililofanyika leo Agosti 12, 2023 katika Viwanja vya Gwambina Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bonanza 2023 Bw. Richard Mauma akizungumza jambo kuhusu Bonanza lililofanyika leo Agosti 12, 2023 katika Viwanja vya Gwambina Jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa TANESCO Wilaya Mbagala Bi. Mariam akizungumzia umuhimu wa kushiriki michezo katika kuongeza ufanisi katika utendaji
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakishindana mbio katika Bonanza lililofanyika leo Agosti 12, 2023 katika Viwanja vya Gwambina Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakishiriki michezo mbalimbali katika Bonanza lililofanyika leo Agosti 12, 2023 katika Viwanja vya Gwambina Jijini Dar es Salaam.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limefanikiwa kuwakutanisha pamoja wafanyakazi wote kupitia Bonanza la Michezo ambalo limelenga kuhudumisha umoja, ushirikiano ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika utekelezaji wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza leo Agosti 12, 2023 Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Meneja wa Wilaya ya Mbagala Mhandisi Elirehema Makacha, amesema kuwa ushiriki wa pamoja kwa wafanyakazi wa TANESCO Wilaya zote nne za mkoa wa Temeke katika michezo unaongeza ushirikiano na kuleta tija ya maendeleo katika utendaji.
Mhandisi Makacha amesema kuwa ni muhimu kushiriki michezo kwani inajenga afya, mshikamano kwa maendeleo ya ushirika.
“Ni utaratibu ambao tumejiwekea kila mwaka tunashiriki michezo mbalimbali kwa lengo la kuleta ufanisi katika utendaji kazi wetu” amesema Mhandisi Makacha.
Amebainisha kuwa TANESCO Mkoa wa Temeke wamejipanga kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake saa 24 ili kuwapatia wateja huduma ya uhakika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bonanza 2023 Bw. Richard Mauma, amesema kuwa miongoni mwa michezo walioshiriki katika bonanza hilo ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa mkono, riadha, kukimbia na magunia, kucheza muziki.
Michezo mingine kukimbiza Kuku, karata, draft, kunywa soda, pamoja na bao.
Nae,mfanyakazi wa TANESCO Wilaya Mbagala Bi. Mariam Manyuka ameupongeza uongozi kwa kutenga muda wa wafanyakazi kupumzika na kushiriki michezo.
“Nimefurahi sana kushiriki bonanza hili kutokana muda mrefu tupo kazini, hatupati nafasi ya kutosha, naomba utaratibu huu mzuri uendelee kila mwaka” amesema Bi. Manyuka.
Hata hivyo Wafanyakazi TANESCO Mkoa wa Temeke wamefuraishwa na utaratibu wa kushiriki michezo mbalimbali kila mwaka kwa kuwa wanadumisha undugu pamoja na kujenga afya imara.