Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Marry Massanja akiangalia bidhaa zinazozalishwa na mazao ya Miti alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Marry Massanja akiangalia bidhaa zinazozalishwa na mazao ya Miti alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Marry Massanja alipotembelea Moja Viwanda vinavyozalisha mazao ya Miti alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii amewataka wamiliki wa Viwanda vinavyozalisha malighafi za misitu katika wilaya ya mufindi mkoani Iringa kutumia Miti iliyofikisha miaka 15 na kuendelea ili kuzalishwa kwa bidhaa za mbao zenye ubora unaotakiwa kimataifa kutoka tanzania.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa maliasili na utalii Marry Masanja alisema kuwa wamiliki na wawekezaji wa viwanda wamekuwa wakinunua bidhaa zisizokidhi vigezo hali ambayo inachangia kuonyesha bidhaa ya misitu kutoka tanzania hazina ubora unaotakiwa kimataifa na kitaifa.
“Nimetembelea viwanda vinne vya wawekezaji ambachonimekiona na naomba sana nielekeze kwa wawekezaji biashara iliyopo ni kubwa sana na viwanda ambavyo nimetembelea ni vikubwa lakini vinaendeshwa chini ya uwezo kwa maana viwanda vina uwezo mkubwa lakini raw material chache nimeona tatizo hili linachangiwa sana na upatikanaji wa raw material zinavunwa zikiwa kwenye umri ambao haujafikiwa na product inayotoka pale inakuwa chini ya kiwango kutokana na gharama kubwa za usafirishaji huku wakikimbilia miti inayouzwa kwa bei rahisi “alisema Marry
Aidha Naibu waziri Marry aliwataka wawekezaji kutumia zao la miti linalopatikana katika shamba za serikali kwani imekuwa ikizalishwa kwa ubora na hitaji la wawekezaji miti iliyokomaa
“Tuna shamba la miti saohill ni shamba zuri na linamiti ambayo imefikia muda wa kuvunwa kwa hiyo niwaombe wawekezaji kwamba pamoja na uanzishwaji wa mashamba binafsi hauzuii serikali kuendelea kulima zao la miti lakini pia pamoja n auhamasishaji tunaofanya wawekezaji waje kuwekeza hatuhamasishi kutumia miti isiyostahili kwa sababu bidhaa itakayotoka hapa itakuwa haina ubora “Marry
Naibu Waziri aliagiza wamiliki wa viwanda kuzingatia haki za wafanyakazi kwa kuwapatia huduma stahiki ikiwa ni pamoja na huduma za kiafya na malipo yao kwa wakati
Tebby Yoram ni Kaimu mkuu wa hifadhi ya misitu shamba la miti la serikali saohill alisema soko la mbao limekuwa na umihimu katika uchumi ,utalii pamoja n auchumi wa viwanda kwani bidhaa nyingi zimekuwa zikizalishwa kutoka huko
“Miaka iliyopita soko la mbao lilishuka kidogo zao hili lina umuhimu katika uchumi wetu kiutalii kwani hapa tuna utalii wa ikolojia pia inatusaidia katika uchumi wa viwanda kwa hiyo ni muhimu sana kuilinda saohill “
Alisema ameyapokea maagizo yaliyotolewa na naibu waziri huku akiahidi kupokea maelekeza na kuyafanyia kazi kama ilivyotakiwa
Kwa upande wao baadhi ya wawekezaji wa viwanda vya uchakataji wa zao la miti wameahidi kufuata maelekezo yaliyotolewa na serikali kwa uaminifu na kununua zao kutoka shamba la miti saohill kwani wanahitaji kuwa wawekezaji wa muda mrefu nawaliomakini katika uwekezaji
“Small farmers is here now but theres verry low quality to compare i have to buy some materials from the government the product is not enough in our Industries because the demand is high”
Ni wajibu wa serikali kuweka sheria ngumu kwa wawekezaji wanaonunua miti michanga kutoka kwa wakulima ili kuruhusu bidhaa ya misitu inayozalishwa kutoka Tanzania kuwa yenye ubora na hata kuipa thamani Tanzania.
MWISHO.