Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Vijana Duniani (UNFPA) Nd. Mark Schreiner akichangia jambo wakati wa kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Mkoani Dodoma (DOYODO) Rajabu Juma akizungumza jambo wakati wa Kongamano hilo.
Sehemu ya Vijana pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu walio hudhuria kongamano hilo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu amesema katika mwaka 2022/23, miradi iliyoibuliwa na vijana 149 imepata mikopo ya Sh. bilioni 3.2 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Akifungua kongamano la kitaifa la vijana katika kuelekea siku ya kimataifa ya vijana Agosti 11, 2023 jijini Dodoma, Prof. Katundu amesema miradi hiyo ni ya kwenye sekta ya kilimo, viwanda, usafirishaji na biashara.
Katibu Mkuu huyo amesema kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 idadi ya vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15-35 ni asilimia 34.5 hivyo wanatakiwa kujengewa uwezo wa kiuchumi.
Naye, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, Zlatan Milisic, amesema kuna umuhimu wa vijana kujengewa uwezo wa kiuchumi kwa kuwa inasaidia kuinua pato la taifa husika.