Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameagiza vyombo vya Usalama kumtafuta Isaya Malogozi (anaedaiwa kuwa mwekezaji) aliye kaidi kuhudhuria Mkutano wa hadhara kutakiwa kutolea ufafanuzi taarifa zake kutaja baadhi ya viongozi wa Wilaya hiyo akiwahusisha katika mgogoro wa ardhi wa muda mrefu baina yake na wanchi.
Amewataka pia Polisi kuachana na tabia ya kuwakamata baadhi ya wananchi katika kijiji hicho kwa madai ya kuagizwa na Issaya Malongoza (anaedai kuwa mwekezaji) mwenye mgogoro na wananchi wa kijiji hicho tangu mwaka 2016.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa maagizo hayo wakati wa mwendelezo wa ziara zake kusikiliza na kutatua Kero mbalimbali za wananchi katika Wilaya ya Same ambapo mara hii ziara hiyo imefanyika katika kijiji cha Nasuro kata ya Bangalala.
Akitolea ufafanuzi mgogoro baina ya wananchi na mwekezaji huyo Mwanasheri wa halmashauri ya wilaya ya Same Upendo kivuyo amesema mwekezaji alienda kijiji jirani cha Bangalala kuomba kuuziwa ardhi kwa ajili ya Uwekezaji lakini Serikali ya kijiji hicho ikauza eneo la kijiji jirani(Nasuro) chenye mgogoro, badala ya kijiji alipo omba.
“Huyu alisha funguliwa kesi ya uvamizi Baraza la ardhi la Wilaya na kijiji kikashinda kesi hiyo hata hivyo mwekezaji alikata rufaa huko pia kijiji kikashinda lakini amekua akiendelea kuwatesa wananchi kwa kukata rufaa hata sasa kuna kesi iko mahakamani”.Alisema Mwanasheri wa halmashauri ya wilaya ya Same Upendo kibungo.
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema tayari katika kesi aliyo fungua mwekezaji huyo mahakama ya mwanzo, wananchi wawili wamefungwa kifungo cha miezi Sita kwa kosa la kuvamiwa eneo hilo ambalo kimsingi wamedai halikuuzwa na kijiji husika.
Kufuatia maelezo hayo Mkuu wa wilaya amemtaka Isaya Malongoza (Mwekezaji) kuacha kufanya shughuli yoyote kijijini hapo mpaka kesi aliyo ikatia Rufaa na Ile aliyo fungua wilayani kumalizika, pia Polisi kumtafuta popote alipo Kwa ajili ya kutoa maelezo ya kukaidi kufika kwenye Mkutano pia kawataja Viongozi wa wilaya anaodai amewaweza mfukoni na kwamba hakuna atakae mgusa wilayani Hapo.