Mhandisi Nedrick Gofrey kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye banda hilo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya
Mtaalam wa Mifumo Bodi ya Mfuko wa Barabara Jastine Govela akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye banda hilo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya katikati ni Agnes Henry katibu Muhtasi kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara
Mhandisi Nedrick Gofrey kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye banda hilo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Kutoka kushoto ni Mhandisi Nedrick Gofrey kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara , Agnes Henry katibu Mhtasi Bodi ya Mfuko wa Barabara RFB, Theresia Mwami Afisa Habari na Jastine Govela Mtaalam wa Mifumo wakiwa katika banda la mfuko huo kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
…………………………………….
Bodi ya Mfuko wa Barabara (RBF), imeendelea kutoa elimu mbalimbali ikiwemo ya mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara kwa wananchi wanaotembelea banda lao katika maonesho ya kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika jijini Mbeya.
Akitoa elimu hiyo Mhandisi Nedrick Godfrey kutoka Bodi ya Mfuko wa Barababara,kwa wananchi waliotembelea katika banda lao amewaeleza juu ya mfumo wa kielektroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara unaowawezesha wananchi kutoa taarifa kwa haraka kupitia simu za kiganjani kwa mamlaka husika kuhusu hali ya barabara ilivyo ili hatua za haraka zichukuliwe.
Hata hivyo uzinduzi wa mfumo wa kieletroniki wa ufuatiliaji wa hali ya barabara nchini ulifanyika jijini Mwanza,Julai mwaka 2022
Sanjari na hayo Mhandisi Nedrick ameeleza kuwa moja ya majukumu ya Bodi ya Mfuko wa Barabara ni pamoja na kukusanya fedha na kupeleka kwa wakala wa barabara nchini na baadae kufuatilia matumizi ya fedha hizo.
Kwa upande wake Mtaalam wa Mifumo kutoka Bodi ya Mfuko wa Barababara Jastine Govela,amewaelimisha wananchi na madereva bodaboda wa jijini Mbeya waliopata fursa ya kutembelea banda hilo juu ya umuhimu wa watumiaji wa vyombo vya moto katika matengenezo ya barabara na namna fedha inayopatikana kupitia watumiaji hao wa vyombo vya moto inavyotumika katika kukarabati miundombinu ya barabara nchini.
“Watumiaji wa vyombo vya moto mnachangia kiasi cha shilingi 263 ya matengenezo ya barabara kutoka katika kila lita ya petroli au dizeli mnayonunua kisha fedha hizo zinapelekwa katika kukarabati miundombinu hiyo ya barabara”.