Mkuu wa wilaya ya same Kasilda Mgeni amewaonya viongozi wa serikali za vijiji dhidi ya tabia iliojikita kwa baadhi yao kutengeneza migogoro hasa ya ardhi ikiwa ni sehemu ya kujipatia kipato.
Kasilda amesema amebaini maeneo mengi yenye migogoro imetengenezwa na baadhi ya viongozi hao kwa maslahi binafsi hali ambayo inapelekea wananchi kutoiamini serikali yao
Ameyasema hayo katika mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza kero za wananchi ambapo wakati huu ameifikia kata ya makanya .
Akihutubia wananchi amesema viongozi hao wajue kuwa wana dhamana ya kuhakikisha wanamsaidia mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samiha Suluhu Hassani kutatua kero zinazowakabili wananchi na si kuwa chanzo cha kero na migogoro kwa wananchi .
Dc Kaslida aliendelea kusema migogoro ya ardhi ambayo wananchi wanailalamikia kwenye kata hiyo kwa kiwango kikubwa imesababishwa na baadhi viongozi wasio waadilifu Kwa kuuza Ardhi kiholela kinyemela huku wananchi wakiendelea kudanganywa kuwa maeneo hayo yamevamiwa na wageni .
Amesema serikali haiwezi kuvumilia kuwa na viongozi wa namna hiyo ,kama hawawezi kubadilika wakae pembeni kabla hawajaondolewa