Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lucas Maganzi akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea katika banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
………………………………
NA JOHN BUKUKU, MBEYA
Wakulima nchini wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika taasisi za fedha ambazo zitawasaidia katika kufanya kilimo cha kisasa ikiwemo kupata mikopo pamoja na kufanya uwekezaji kwa kununua hati fungani.
Akizungumza katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Lucas Maganzi, amesema kuwa wakati umefika kwa walikuwa kuanza kutumia taasisi za fedha ili kupata fursa zilizopo.
Bw. Maganzi amesema kuwa ili kuwafikia watu wengi wamekuwa wakishiriki maonesho mbalimbali wakiwa na lengo la kutoa elimu ya fedha kwani umuhimu katika shughuli za maendeleo.
“Kuna wakati mkulima anakuwa na pesa nyingi, lakini hajui wapi akawekeze, hivyo tupo nanenane kwa ajili ya kutoa elimu, ushauri kuhusu umuhimu wa mazao kuwa na bima”
Amesema kuwa BoT wana utaratibu wa kutoa mikopo na kumdhamini mtu kuanzia asilimia 50 hadi 75 kwa ajili ya kuwasaidia ili ambao hawana vigezo vya kupata mkopo wapate na kufikia malengo yao.
Amefafanua kuwa lengo ni kuhakikisha mpaka kufikia mwaka 2028 asilimia 99 ya watanzania wawe wanatumia huduma za kibenki ambazo zipo rasmi.
Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lucas Maganzi akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea katika banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lucas Maganzi akielezea mambo mbalimbali kuhusu shughuli za benki hiyo.
Afisa Sheria Mwandamizi, Kurugenzi ya Huduma Sekta ya Kifedha, Ramadhani Myonga na Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lucas Maganzi wakipozi kwa picha.