Afisa Uhusiano Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Renatus Sona akizungumza katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Mtonyi Chilala Msanifu Majengo wa TBA akitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Cecilia Ndumbaro Mbunifu Majengo wa Wakala wa Majengo TBA akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la TBA ili kupata ufahamu wa shughuli za taasisi hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Haruna Kalunga Mhandisi Majengo TBA akiwasimamia watoto wakati wakijaza majina yao katika kitabu cha wageni walipotembelea banda la TBA katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
Pendo Palyani Afisa Mawasiliano TBA akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika katika banda la TBA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ya serikali.
……………………………….
Wakala wa majengo Tanzania (TBA)wametoa Rai Kwa wananchi kujitokeza kwenye maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya ili kujifunza na kutambua shughuli zinazofanywa na wakala hiyo lakini pia kupata ushauri wa namna ya kufanya ujenzi Bora na Kwa bei nafuu.
Akizungumza Leo Agosti 5, 2023 kwenye Banda lao lililopo kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane Afisa Uhusiano wa TBA Renatus Sonna amesema wamekuwa wakishiriki katika ujenzi wa miliki za serikali ikiwemo ujenzi wa ofisi za serikali na makazi ya watumishi wa umma.
“TBA ni taasisi ya serikali kazi yetu kubwa ni kuanzisha, kusimamia na kuendeleza miliki za serikali yaani nyumba,viwanja,majengo na hata mashamba”amesema Sonna
Aidha ameongeza kuwa TBA imekuwa na miradi mbalimbali ya mkakati Inayoendelezwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo mji wa kiserikali Mtumba mkoani Dodoma ambapo TBA wamekuwa washauri elekezi kwenye mradi huo
Amesema katika mradi huo wa mji wa serikali TBA ni washauri elekezi wanasimamia lakini wanajenga wizara Moja jengo la Wizara ya Ofisi ya Rais Utawala Bora na utumishi wa umma.
Sambamba na hayo Sona amesema ushiriki wao kwenye maonyesho hayo imetokana na kuwa wadau wa kilimo Kwani wameshiriki kwenye ujenzi wa maghara ya kuhifadhia chakula maarufu kama vihege ambao umejengwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Arusha,Njombe na Makambako.