Na Sophia Kingimali
Kufuatia juhudi zanazofanywa na Rais Samia Suruhu Hassan za kuipeleka nchi kimataifa zimepelekea Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuibuka na ushindi wa kuwa makamu mwenyekiti kwenye shirika la umoja wa mataifa la utalii Kanda ya Afrika(UNWTO)
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Agosti 5 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Hassan Abas amesema kutokana na mkutano huo umeonyesha juhudi kubwa zilizofanywa na serikali katika uwekezaji..
Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana kutokana na mkutano huo amesema Tanzania imefanikiwa kushinda nafasi ya makamu mwenyekiti wa shirika la utalii ngazi ya dunia ambapo imekua miongoni mwa nchi mbili za Afrika zitakazoliwakilisha bara la Afrika kwenye Baraza kuu la shirika la italii Duniani.
Aidha Dkt Abas amesema pia Tanzania pia imechaguliwa kuingia kwenye kamati tendaji ya Baraza Hilo ambapo nchi 13 ziligombea wakati nafasi zilikua sita na Tanzania kuingia kwenye nafasi hizo sita zilizoshinda.
Amesema kuingia kwenye kamati tendaji hiyo ni fursa Kwa nchi kupata miradi mbalimbali itakayokuwa inatolewa na shirika hilo la utalii la Dunia.
Sambamba na hayo Dkt Abas ameongeza kupitia mkutano huo wa 66 Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili yenye watalii wengi katika robo ya kwanza huku ya kwanza ikiwa Ethiopia na ya tatu Morroco.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Bodi ya autalii Damas Mfugale amesema wanapaswa kutumia ushindi huo kama fursa ya kuboresha mahusiano katika sekta ya utalii illi kuvutia utalii zàidi na kutangaza vivutio.
“Tanzania inaheshimika sana kimataifa tunapaswa kuboresha mahusiono yetu ili kuvutia utalii tusitegemee tu watalii wawe wazungu lakini pia tunaweza kuvutia utalii katika nchi zetu za Afrika”amesema Mfugale
Kwa upande wake mkurugenzi wa utalii kutoka wizara ya Mali asili na utalii Bi. Theresa Mugori ametoa wito Kwa wawekezaji kujitokeza kuwekeza kwenye miundombinu ya vivutio ili kuzidi kuboresha sekta hiyo.
“Tumeenda kwenye mkutano lakini tumepata nafasi ya kujifunza namna wenzetu wanavyofanya kwenye utalii tumeona wamewekeza sana kwenye miundombinu yao Hali iliyopelekea kuvutia utalii.
Sambamba na hayo Mugori amesema sekta ya utalii inakua Kwa kuwashirikisha sekta binafsi hasa katika utafiti hivyo serikali imejipanga kulitekeleza swala Hilo.
Tanzania ilishiriki kwenye mkutano wa Kanda ya Afrika katika mkutano mkuu wa Dunia wa shirika la utalii Duniani(UNWTO) uliofanyika katika nchi ya Mauritania Julai 26 2023 ambapo Tanzania ni mwanachama hai Kwani shirika Linawanachama 160 huku likiwa na Kanda 6 ambapo lilianzishwa mwaka 1974 na Tanzania kujiunga 1975.