Mafuta aina yanayotokana na Mmea wa Mchaichai ambayo yamefayiwa utafiti na wataalam wa TIRDO yakioneshwa kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofayika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mtaalam na Mtafiti kutoka Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO ) *Bwana Paul Josephat Kimath akizungumza na wananchi waliofika kwenye banda la TIRDO kujionea bidhaa mbalimbali ikiwemo ya mafuta Tete (Essential Oil) zilizofanyiwa utafiti na kuzalishwa na shirika la TIRDO katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofayika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Mmea wa Mchaichai ambao umafanyiwa utafiti na kuzalishwa mafuta Tete (Essential Oil).
…………………………….
Mchaichai ni mmea unaofahamika kwa watu wengi katika mazingira yetu ya asili na kwa muda mrefu mmea huu umetumika kama kiungo kwenye kinywaji (chai ) kutokana na ladha na harufu yake nzuri.
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) wamekuja na utafiti uliofanikisha kupatikana kwa mafuta tete (Essential Oil) yanayotumika kama malighafi ya viwandani na tiba kwa magonjwa mbali mbali.
Mtaalam na Mtafiti kutoka Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO ) *Bwana Paul Josephat Kimath* anasema mafuta yanayotokana na mmea huo yana faida nyingi ikiwa ni pamoja na kutibu vidonda vya tumbo, kinga ya saratani , kuondoa sumu mwilini pamoja na kusafisha figo.
Bwana Kimath anasema kuwa baada ya kugundulika kuwa mmea huo una faida nyingi wataalam kutoka TIRDO tulifanya utafiti wa kutengeneza mashine ya kuchakata mafuta ya mchaichai.
‘”Tunamshukuru sana mkurugenzi wetu *Prof.Madundo Mtambo* ambaye mara zote amekuwa akitusimamia na kuhakikisha tunakuja na teknolojia zinazotatua changamoto katika jamii yetu’’ aliongeza Bw.Kimath.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TIRDO *Bwana David Langa* alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau wa uwekezaji katika sekta ya Viwanda kufika katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya na katika ofisi zao zilizopo Msasani Jijini Dar Es Salaam kutumia fursa za kitafiti zinazopatikana katika shirika hilo.
“Sisi kama shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda nchini tuna jukumu la kufanya utafiti na baada ya kuthibitika tunazitoa kwa wananchi ili waweze kuzitumia kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu’’ aliongeza Bw.Langa.