Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed, akipokea maelezo kuhusu mfumo wa kusajili na kuhifadhi kumbukumbu za wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka kwa mtaalam wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa chama hicho wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa linaloendeshwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar-es-Salaam.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed, akiagana na Katibu wa Baraza la Wazee wa chama cha CHADEMA ndugu Rodrick Rutembeka baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa linaloendeshwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar-es-Salaam.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed, akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo Magomeni jijini Dar-es-Salaam leo. Naibu Msajili Ahmed kwenye ziara yake alipokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Ado Shaibu.
Naibu Msajili wa Vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed, akipokea maelezo ya moja ya picha zilozobandikwa kwenye kuta za ukumbi wa mikutano wa chama cha ACT Wazalendo kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Ado Shaibu. Naibu Msajili Ahmed leo amefanya ziara fupi kutembelea vyama vya CHADEMA, CCK na ACT Wazalendo.