Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania,TASAC Bi. Martha Calvin akizungumza na wananchi mbalimbali hawapo pichani waliotembelea katika banda la TASAC kwenye maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Johm Mwakangale jijini Mbeya.
…………………….
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania,TASAC ni kati ya Taasisi nyingi za Kiserikali zinazoshiriki Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima yanayotambulika kama NaneNane.
Maonesho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya yameanza Agosti 1, 2023 na kilele chake kitafanyika Agosti 8, 2023.Kauli mbiu ya maonesho hayo ni ikiwa ni “Tanzania: Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo ya Chakula na Usalama wa Chakula ”.
TASAC inashiriki maonesho hayo ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanayotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415.
TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea banda la TASAC ambalo lipo katika eneo zilipo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi wananchi wote wanakaribishwa kutembelea katika banda hilo ili kupata elimu na uelewa kuhusu shughuli mbalimbali za TASAC.
Mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania,TASAC akisaini kitabu cha wageni kwenye maonesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Johm Mwakangale jijini Mbeya kulia ni . Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC Bi. Martha Calvin na katikati ni Abubakari Waziri Afisa Uhusiano kwa Umma TASAC.