NJOMBE, Kufuatia Wananchi wa Kata ya Ikondo Jimbo la Lupembe Kufuata huduma za Afya Kwa Umbali Mrefu wa Zaidi ya KM 30 kwa Miaka Mingi Serikali Wilayani Njombe Imeanza Rasmi Ujenzi was Kituo cha Afya ili Kutatua Kero ya Muda Mrefu ya Kufata Matibabu Kata Jirani.
Kuanza Kutekelezwa Kwa Mradi huo Kunamuibua Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Swalle kutembelea na Kisha Kufanya Ukaguzi ili kujua Maendeleo ya mradi Huo ambapo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imedhamilia Kuboresha Huduma za Afya ili Kuhakikisha Kuokoa Vifo Visivyo vya Lazima Vikiwemo Vya Mama na Mtoto Wakati wa Kujifungua.
Mara Baada ya Ukaguzi Mbunge Swalle Anatoa Rai kwa Wananchi wa kata ya Ikondo kuhakikisha Wanalinda Miundombinu ya Mradi huo na Mingune Yote Inayotekelezwa katika Kata yao Ili Waweze Kupata Tija Katika jamii.
Kwa Upande wake Diwani wa kata ya Ikondo Milius Lupenza anakiri Kuwa Wananchi wa kata Hiyo Wamekuwa Wakifuata Huduma za Afya kwa Umbali Mrefu na Kwamba Kukamilika kwa Mradi huo Kutakuwa na Matokeo Chanya Kwa Wananchi.
Nao Wananchi akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikondo Ayubu Mhelela amesema Wananchi wa Kata ya Ikondo Wanakwenda Kunufaika moja Kwa moja Mradi huo huku Pia Akisema Katika Utemelezaji Wake Wananchi Wameshirik Kikamilifu.
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Enosy Swalle ameaandelea na Ziara ya Kikazi Jimbo ikiwa na Lengo la Kusikiliza Kero na Changamoto za Wananchi ili Kuzitafutia Ufumbuzi na Kisha kutoa Mrejesho wa Utemelezaji Wa Ahadi Zake.