…………………
Na. Sixmund J. Begashe
Hifadhi ya Taifa Ruaha imeendelea kuwa kivutio kikubwa cha Watalii wa ndani na nje ya nchi kutokana na Vivutio vya kila aina hususani makundi ya Falimia jamii ya paka kama Simba wenye idadi ya simba 40, Utalii wa Usiku na Mchana, Utalii wa Miguu hali inayomfanya Mtalii kukaa siku zaidi ya Moja Hifadhi humo.
Akieleza kwa furaha namna alivyo furahia Utalii ndani ya uhifaji hiyo, Mtalii kutoka Ufaransa Bi. Ines Richard, amesema imekuwa ni zaidi ya matarajio kwa kuwa licha ya kuona makundi Makubwa ya Simba, pia ameweza ameona Wanyama wakubwa na wadogo, ndege zaidi ya aina 570 na mimea ya Kila aina.
Akizungumzia Hifadhi hiyo, Muhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Godwell Ole Meng’ataki, ameeleza kuwa Hifadhi hiyo imekuwa kimbilio la Watalii wengi kutokana na Utajiri wa Vivutio kwenye hifadhili, Malazi, vyakula vya bei rafiki, uvuvi wa Kitalii nk.
Aidha Kamishna Msaidizi Mwandamizi Godwell Ole Meng’ataki, ameongeza kuwa Hifadhi hiyo ya pili kwa Ukubwa nchini, imekuwa kivutio kikubwa kutoka kuwa na Miundombinu mzuri hususani baraba ndani ya Hifadhi kupitia Mradi wa kukuza na Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW).
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Godwell Ole Meng’ata ameongeza kuwa, kupitia Mradi huo wa REGROW, Hifadhi hiyo inatekeleza ujenzi wa Kiwanja Cha ndege, Barabara ndani ya Hifadhi, Uchimbaji wa Mabwawa 32 kwa ajili ya Wanyama, ujenzi wa sehemu za Malazi, Kituo cha Utafiti, Sehemu Kwa ajili ya Ulinzi wa Maliasili nk.