Na John Walter-Manyara
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara wamemchagua Yahaya Hamisi Loya Diwani wa kata ya Ayasanda kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa mwaka mpya wa fedha 2023-2024.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika leo Julai 28,2023 katika kikao Cha baraza la Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo amesema kura 32 kati ya 33 zilisema ndio na Moja hapana.
Makamu Mwenyekiti mteule Yahaya Hamisi Loya amewashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpitisha kwa kishindo huku akisema kura Moja ya hapana alijipigia yeye.
Ni uratatibu wa kawaida kuchagua makamu Mwenyekiti kila baada ya mwaka Mmoja huku Mwenyekiti akichaguliwa kila baada ya miaka mitano, ambapo aliyepitishwa hakuwa na mpinzani kwa kuwa baraza Hilo lina Madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) pekee.