RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Naibu Mifti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi alipowasili katika viwanja vya Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika msikiti huo leo 28-7-2023.(Picha na Ikulu).
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia Wananchi,baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja leo 28-7-2023 Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 28-7-2023.(Picha na Ikulu).
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakishiriki katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 28-7-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuina na Viongozi na Wananchi katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na (kushoto kwa Rais) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid.(Picha na Ikulu)