Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba alipotembelea banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika maonesho ya biashara kimataifa SABASABA yanayofanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Mkurugenzi wa huduma kwa mlipa kodi (TRA) Bw. Richard Kayombo wakiangalia jinsi ya kuskani kinywaji kwa njia ya mfumo wa kielektroniki (ETS) unaotolewa na kampuni ya SICPA ili kuhakiki stempu na kuhakikisha kinywaji ni salama kwa matumizi ya binadamu katika kampeni iitwayo “Hakiki Stempu, Linda Afya yako”.
Mkurugenzi wa mambo ya ndani kutoka TRA Bw. Ndositwe Haonga akipewa maelekezo na afisa wa TRA juu ya matumizi ya mfumo wa kuhakiki stempu kielektroniki (ETS) unavyofanya kazi katika kuskani stempu za vinywaji kama maji, juice, pombe kali na sigara, pindi alipotembelea banda la mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) katika maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara katika viwanja vya sabasaba yanayofanyika mwezi July kila mwaka jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala Bw. Moshi Kabengwe kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) alipotembelea banda la TRA katika maonesho ya kimataifa ya biashara Sabasaba, akiwa pamoja na afisa kutoka TRA wakiskani stempu katika kinywaji kwa njia ya kielektroniki ili kuhakiki kama kinywaji hicho ni salama kwa matumizi ya binadamu na kusaidia kulinda afya ya watumiaji. Mfumo wa kuhakiki stempu kielektroniki (ETS) unaotolewa na kampuni ya SICPA ni mfumo uliosaidia na kuleta manufaa katika ukusanyaji wa kodi na mapato nchini Tanzania.
Afisa kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Ben Makobwe akiskani stempu ya kinywaji kwa njia ya kielektroniki ETS (Electronic Tax Stamp) katika maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara Sabasaba yanayofanyika July kila mwaka jijini Dar es Salaam.