Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Regine Hess.
Waziri Aweso na Balozi Regine Hess wamezungumzia maswala kadha ya kadha kuhusiana na Mashirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Ujerumani katika sekta ya Maji miradi ya kimkakati.
Pamoja na mambo mengine Waziri Aweso na timu ya wataalamu Wizara ya Maji wakiongozwa na Katibu Mkuu Eng Nadhifa Kemikimba wamezungumzia mikakati ya kuendeleza ushirikiano katika Utekelezaji wa Miradi ya Maji ambayo tayari ipo katika hatua mbalimbali.