Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekutana na kufanya mazungumzo ya kimkakati na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima leo Julai 26,2023 Mkoani Morogoro.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili na kuweka mikakati ya ushirikiano wa pamoja kwenye shughuli za uhifadhi wa maeneo yanayosimamiwa na TAWA ndani ya Mkoa wa Morogoro ambayo ni pamoja na Mapori ya Akiba ya Kilombero na Wamimbiki.
Kikao hiko kilijumuisha pia Wakuu wa Wilaya watano (5) wanaozunguka Mkoa wa Morogoro ambao ni Rebecca Sanga Nsemwa (Morogoro), Dkt. Julius Kenneth Ningu (Ulanga), Judith Martin Nguli (Mvomero), Sebastian Muungano Waryuba (Malinyi) na Dastan Dominic Kyobya (Kilombero).
Ujumbe kutoka TAWA uliongozwa na Kamishna wa Uhifadhi, Mabula Misungwi Nyanda.