Taasisi za Uhifadhi za TAWA, TANAPA na TAWIRI zikishirikiana na Uongozi wa Wilaya ya Bunda wametekeleza kazi ya udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu hususani Tembo katika Wilaya ya Bunda DC kwa kutumia Hedikopta.
Lengo ni kutekeleza mkakati wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa kutatua kero za wanyamapori sambamba na Utoaji Elimu kwa wananchi juu ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.
Uwepo wa Matumizi ya Teknologia katika udhibiti wa Tembo na wanyamapori wakali na waharibifu Umesaidia kufanikisha Makundi manne ya tembo kufukuzwa kutoka katika vijiji Vinne ambavyo ni Sarakwa, Nyatwali, Lukungu na Tairo na kurudishwa ndani ya hifadhi.
Aidha, kundi moja limewekewa kisukuma mawimbi (GPS) kwa lengo la kusaidia kuzuia Tembo kutofanya uharibifu vijijini kabla ya Askari wa Uhifadhi kupata taarifa kwa wakati.