Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) imeziagiza taasisi za umma kuhakikisha watumishi wote wanaohusika na ununuzi wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuutumia mfumo mpya wa ununuzi “National e-Procurement System of Tanzania” (NeST).
Agizo hilo limetolewa na PPRA kupitia taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo hivi karibuni, ambapo taarifa hiyo imesema kuwa, taasisi za umma zinawajibu wa kuhakikisha watumishi wote wanaohusika na ununuzi wamepatiwa mafunzo.
Aidha, taasisi hizo zimetakiwa kuhuisha watumiaji kwa wakati pindi wanapoondoka kwenye taasisi kwa sababu yoyote.
Wajibu mwingine wa taasisi hizo katika mfumo huo mpya ni kuhakikisha uandaaji wa bajeti hususani bidhaa na huduma zitakazonunuliwa umefanyika kwa uhalisia ili waweze kutengeneza mpango wa ununuzi uliosahihi.
Vile vile Kuhakikisha uandaaji wa bajeti hususani bidhaa na huduma zitakazonunuliwa umefanyika kwa uhalisia ili waweze kutengeneza mpango wa ununuzi uliosahihi.
Sambamba na hayo taasisi za umma zimetakiwa kuhakikisha uandaaji wa bajeti hususani bidhaa na huduma zinatakazonunuliwa umefanyika kwa uhalisia ili waweze kutengeneza mpango wa ununuzi uliosahihi.
Mfumo mpya wa ununuzi “National e-Procurement System of Tanzania” (NeST) umeanza kutumika rasmi Julai mwaka huu, ambapo taasisi zimetakiwa kutengeneza Mpango wa Ununuzi wa Mwaka ili ziruhusiwe kutumia mfumo huo.