Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi Vyandarua Mkuu wa Kaya ya Matarumbeta ZONE “A” katika Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua Vyenye Dawa kwenye Kaya,hafla iliofanyika Shehia ya Matarumbeta Wilaya ya Mjini Unguja.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua Vyenye Dawa kwenye Kaya,hafla iliofanyika Shehia ya Matarumbeta Wilaya ya Mjini Unguja.
Na Rahma Khamisi Maelezo 25/7/2023
Wananchi wametakiwa kuvitumia kwa usahihi vyandarua watavyopewa serikali dhidi ya ugonjwa wa malaria ili kujikinga na maambukizi ya mbu wa Malaria.
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Mjini katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Ugawaji wa vyandarua vyenye dawa huko Uwanja wa Matarumbeta, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema Amesema
vyandarua hivyo vyenye dawa vinadumu kwa muda wa miaka 3na vinatolewa kwa wananchi wote nchini.
Amesema vyandarua hivyo vitagawiwa kwa wote nchini vitasaidia kuzuwia maabukizi hivyo ni vyema kuvitumia kwa usahihi ili serikali ipate kufikia lengo la kutokomeza ugonjwa huo.
Fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuwalinda na kuwahifadhi wananchi dhidi ya mbu wa malaria.
“Vyandarua hivi tunavitoa kwa matumizi ya binadamu na si vyenginevyo ,hivyo lazima tuvitumie katika njia sahihi iliyokusudiwa ”, alifahamisha Waziri.
Amefahamisha kuwa malaria bado yapo nchini hivyo amewasisitza wananchi kujitahidi kuhifadhi mazingira kwa kufanya usafi kila sehemu ili kujikinga kwani Mazingira machafu ndio yanapelekea mazalia ya mbu anaesababisha malaria.
Waziri Mazrui ameeleza kuwa jumla ya watu 3373 waliripotiwa kupata malaria na watu sita kufariki dunia hivyo kutokana na hali hiyo Wizara inaswaisitiza wananchi kuendelea kutumia vyandarua watakavyopatiwa kwani kila mmoja ana jukumu la kutoa mchango wake kuondosha malaria .
“ Takwimu zinaonesha dhahiri kuwa malaria yapo Zanzibar kwani kwa mwaka huu ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu sita tena vijana wadogo hii ni ishara mbaya na nidhahiri kuwa malaria hayajaondoka ,”Waziri aliwasisitiza wananchi.
Aidha Waziri ameongeza kuwa asilimia 46 ya wakaazi ni kutoka Mkoa wa Mjini hivyo vyandarua vitaanza kutolewa katika Mkoa huo ambao una wakaazi wengi wanaotoka maeneo tofauti .
Katika hatua nyengine Waziri amesema kuwa Serikali inapambana kuhakikisha wananchi wake wanapata afya bora, ni jukumu la kila mtu kutoa mchango wake ili Zanzibar ibaki salama kwani bila ya malaria inawezekana.
Waziri Nazrui amewataka wananchi kufuatilia terehe za ugawaji wa vyandarua na kufika vituoni mapema kwa ajili ya kuchukua vyandarua vyao na kuvitumia kwa usahihi.
“Nawaomba wale waotoaji wa vibali vya ujenzi wa nyumba kuhakikisha wanatoa kwa kuzingatia maadili ya afya na mazingira kwani nyumba nyingi zinayojenwa hazifuati masharti ya ujenzi na kupelekea kuwepo na mazingira hatarishi ma kupelekea mbu kuweka makaazi yao” alieleza Waziri Mzrui.
Akitoa taarifa kuhusiana na ongezeko la ugonjwa huo Meneja wa Kitengo cha kuzuwia Malaria Zanzibar Shija Joseph Shija amesema kuwa kuanzia January hadi June Wilaya ya Mjini na Wilaya ya Magharib “B” ndizo zinazoongoza ikifuatiwa na Wilaya ya kusini kwasababu ya wananchi hao kuchelewa kufika hospitali mapema.
Ameeleza kuwa takwimu zinaonesha wanaoathirika na ugonjwa huo zaidi ni vijana ,wanafunzi wasafiri na wanaofanya biashara ambao watembea maeneo tofauti.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Msaraka amewataka wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa usahihi na kuvitunza kufikia leno lilikusudiwa la kutokomeza malaria nchini.
Amesema kuwa serikali imeanzisha mpango wa kufanya usafi kila mwisho wa mwezi ili kutokomeza mazalia ya mbu yasienee katika jamii.
Nae Muwakilishi kutoka Marekani ambae pia Naibu Mkuruenzi wa CDC Anna Hothmen amewataka wananchi kuacha tabia ya kutumia vyandarua katika shuhuli za uvuvi na kujengea bustani na badala yake kuvitumia katika matumizi sahihi ili kujikinga na maambukizi .
Zoezi la ugawaji wa vyandarua vilivyotiwa dawa linatarajiwa kuanza rasmi kesho tarehe 26 Julai mwaka katika Shehia 53 za Wilaya ya Mjini na limeandaliwa na Wizara ya Afya chini ya ufadhiliwa wa Wadau mbalimbali wa Maendeleo wakiwemo USAD , CDC, GLOBALFOUND na BREAKTHROU ambapo jumla ya Tsh 430,o47zimetumika katika mradi huo.