Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mh. Omary Kipanga akimkabidhi cheti cha ushiriki wa maonesho ya Vyuo Vikuu Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha baada ya chuo hicho kushiriki maonesho hayo yaliyomalizika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Leo Julai 22, 2023.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Leo Julai 22, 2023.
……………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Chuo Kikuu Mzumbe kimejipanga kuendelea kukuza na kuzalisha vipaji kupitia programu mbalimbali wanazofundisha Chuo hapo katika kuhakikisha mwanafunzi anafikia malengo tarajiwa pamoja na kuwa na uwelewa mkubwa baada ya kuhitimu.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, maonesho ya 18 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2023, yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha, amesema kuwa Chuo Kikuu Mzumbe kuna programu maalamu za kulea bunifu ili kuleta tija na ufanisi katika maendeleo ya nchi.
Profesa Mwegoha amesema kuwa wamekuwa na utaratibu kwa wanafunzi kufanya mazoezi ya vitendo kwa muda mrefu jambo ambalo limeleta mafanikio makubwa kwa kuzalisha wanafunzi wenye uwezo mkubwa.
“Wapo viongozi wengi wamesoma Chuo Kikuu Mzumbe, sisi tunafundisha vitu vingi ikiwemo maadili katika kuhakikisha mtu anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi” amesema Profesa Mwegoha.
Hata hivyo amebainisha kuwa mwaka wa jana wamedahili wanafunzi 13, 735, idadi ambayo imekuwa ikiongezeka kadri kila mwaka.
“Ni matokeo mazuri yaliotokana na juhudi katika kutangaza programu zetu ikiwemo sheria na utawala” Profesa Mwegoha.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Mipango Fedha na Utawala Prof. Allen Mushi akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Chuo hicho waliokuwa wakishiriki kutoa Elimu na kuwafanyia usajili wanafunzi wanaotarajia kujiumga na Chuo hicho kwenye maonesho ya vyuo Vikuu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Maonesho hayo yanaandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU.