………………..
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Ladislaus Chang’a amekabidhi magari nane (8) kwa vituo vya Dodoma (Makao Makuu),Arusha, Mbeya, Kilimanjaro (KIA), Mwanza,Zanzibar, Morogoro, Iringa na Dar es Salaam (JNIA) kwa wakuu wa vituo na madereva.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Dkt. Chang’a alitoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa kuendelea kuimarisha vitendea kazi na miundombinu ya utoaji wa huduma katika TMA na kuwasisitiza madereva hao kuyatunza magari waliyoyapokea kwa manufaa ya watumishi wote, Mamlaka na Taifa kwa ujumla
Aidha, Dkt. Chang’a aliwaagiza mameneja wa vituo, kusimamia ipasavyo matumizi ya magari hayo na kuhakikisha kuwa magari hayo yanatotumika kwa shughuli za kiofisi na za uendeshaji wa vituo na si vinginevyo.
Awali, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi TMA, Ndg. Braison M. Kunyalanyala aliwasisitiza madereva kuwa waadilifu kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya taratibu za serikali na kutambua kuwa magari hayo ndio ofisi zao, hivyo wanatakiwa kuyatunza ili kuipa umuhimu na thamani kazi yao.