Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye akizungumza katika kikao hicho jijini Arusha leo.
……
Julieth Laizer ,Arusha .
Arusha.Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye,amewataka watendaji wa wizara hiyo kusimamia vipaumbele waliyojiwekea katika mwaka wa fedha ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa urahisi.
Waziri Nape ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu cha viongozi wa wizara na taasisi zilizochini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Amesema serikali inafanyia kazi malalamiko ya gharama za mawasiliano ili kila mtanzania apate huduma bora na rahisi.
Ameongeza kuwa, watanzania wanastahili huduma bora za mawasiliano na rahisi zinazopatikana kila mahali na kuwa miongoni mwa vipaumbele vya mwaka huu wa fedha ni kuanza kurusha satelaiti hiyo itarahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini.
“Tunatakiwa tukae na kutafakari namna bora baada ya Bunge na Rais kufanya maamuzi kadhaa ambayo yatatupeleka kwenye kuangalia namna huduma hizi zitaboreka,rahisi na zinazopatikana tunategemewa kutoka na majawabu hapa na wizara ndiyo inawezesha wizara zingine kufanya kazi tunayo kazi kuhakikisha tunatoka na mambo ambayo yatakwenda kusaidia,”amesema
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mohamed Khamis Abdulla amewataka watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa kujituma bila kushurutishwa na kushirikiana na kuwatama wakuu wa taasisi kusimamia urekelezaji wa sera, kanuni,miongozo,taratibu na utawala bora .
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar,Shomari Omari Shomari,amesema ushirikiano baina ya pande hizo mbili zinasaidia kuboresha muungano na kuongeza kasi ya uchumi wa kidigitali