…….,……
Dar es Salaam, 19Julai,2023:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa juu ya mwenendo wa uwepo hali ya El Niño katika bahari ya Pasifiki na athari zake nchini.
Kwa Mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na Mamlaka hiyoleo imeeleza El Niño ni mfumo wa hali ya hewa unaosababishwa na uwepo wa ongezeko lajoto la bahari la juu ya wastani katika eneo la kati la kitropiki la bahari ya Pasifiki.
Hali hio huambatana na athari mbalimbali ikiwemo ongezekola mvua, joto na hali ya ukame katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Aidha, ukubwa wa athari hizo unategemea nguvu pamojana muda ambao hali ya El Niño itadumu, na pia inategemea hali na mwelekeo wa mifumo mingine ya hali ya hewa ikiwemomwelekeo wa upeopo na jotola bahari katika Bahari ya Hindi.Kwa Tanzania, hali yahii ya El Niño huambatana na vipindi vya mvua kubwana za juu ya wastani.
Mamlakaimeendelea kufuatilia mwenendowa mifumo ya hali ya hewa kiwemo El Niño.
Kwa ujumla mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuanza kujitokeza kwaEl Niño,hali ambayo inatarajiwa kuimarika zaidikuelekea mwishonimwa mwaka2023.Uchambuzi waawali wamifumoya hali ya hewa unaonesha kuwa El Niñoitakuwa nanguvu ya wastani.
Hata hivyo,athari za moja kwa moja hazijaanza kujitokeza katika maeneo ya nchi yetu kwa kipindi hiki cha Kipupwe.
Aidha, Mamlaka imeendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo mbalimbali ya hali ya hewa kwa ukaribuna kufanya uchambuzi wa kina utakaoainisha athariza El Niñokatika mifumo ya mvua hususanmsimu wa mvua za Vuli(Oktoba hadi Disemba),2023na taarifa hiyo itajumuisha ushauri stahiki kwa sekta mbalimbalina itatolewa kablaya kuanza kwa msimu.
Kwa upande mwingine, msimu wa Kipupwe(Juni-Agosti), 2023bado unaendeleakama taarifaya utabiri ilivyotolewa mwezi Mei, 2023.Vipindivya upepo mkali pamojana baridi vimeendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Hali yabaridi kali imeendelea kujitokeza katika maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi(ikijumuisha mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa)na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Katika kipindi cha mwezi Julai, 2023 kiwango kidogozaidicha joto la chini cha nyuzi joto 2.50C kimeripotiwa katika kituo cha Uyole, Mbeyamnamo tarehe 5 Julai, 2023.
Kwa taarifa hii wananchi wanashauriwa kuendelea kuzingatia taarifa na tahadhari za hali mbayaya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania sambamba na kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazotokana na hali mbaya ya hewa.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewakwa ujumlana kutoa mrejeo kila itakapobidi.