Mbunge wa Tanga mjini Mhe.Ummy Mwalimu Leo tarehe 18/7/2023 ametembelea kata ya Ngamiani Kusini na kupokea utekelezaji wa ilani wa 2022/2023 katika kata hiyo.
Pia mheshimiwa mbunge amepokea changamoto zilizopo katika kata hiyo ikiwemo miundo mbinu ya maji taka udogo wa eneo la shule ya msingi Ngamiani kusini.
Mhe mbunge ummy mwalimu amepokea changamoto hizo na kuaidi kuzifanyia kazi Ili kuweza kuimariisha miundo mbinu hiyo Kwa kushirikiana na Tanga uwasa na serekali.
Katika ziara hiyo mhe.mbunge ameongozana na mhe.diwani wa kata hiyo mhe.Mtanga Aweso
Imetolewa na;
Ofisi ya mbunge Jimbo la Tanga mjini
18/7/2023