Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan akimpokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Hungary Mheshimiwa. Katalin Novák wakati alipowasili Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo mwenyeji wake.
Rais Katalin Nová yuko nchini kwa ziara ya siku mbili ya kikazi ambapo yeye namwenyeji wake Rais Dkt Samia Suluhu Hassan leo Julai 18, 2023 watashuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano (MOU) katika masuala ya elimu.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-IKULU
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati Rais wa Hungary Mheshimiwa Katalan Novac alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Julai 18,2023.