Na Ahmed Mahmoud
Rai imetolewa Kwa Watanzania kuanza kubadilika katika suala Zima la Lishe Kwa mbegu lazima ionyesha ina mchango upi katika eneo la Lishe Kwa Sababu lishe ni jambo mtambuka ambalo linaanza kutazamwa na serikali kwa jicho tofauti.
Kwa Muktadha huo jamii kuanza kubadilika wewe kama mkulima au mlaji unapoenda sokoni kununua au kuuza mazao lazima uulize au ueleze Faida inayopatika kwenye Maharagwe unapata Nini humo ndani unapokuwa unakula na familia yako Ili tuweze kujenga Taifa lenye Afya bora kuondoa changamoto za kiafya.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mali Daniel Leiruk wakati akifunga maonesho 11 ya siku mbili ya kilimo biashara yalioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa kilimo TARI-Selian Jijini Arusha.
Alisema kwamba Serikali ndio maana imetenga bajeti kubwa katika mwaka huu wa fedha 2023/24 kumekuwa na ongezeko la Takribani Bilion 970 Kutoka bilion 750 ya Mwaka uliopita wa fedhà ikiwa ni kuimarisha miundombinu katika mnyororo wa thamani ya mazao ya kilimo.
Kwa mujibu wa Leiruk Kwa hiyo tunapaswa Sasa kuamka na tunaposema kilimo Cha kibiashara hakikisha kwamba Mtu mojamoja hatusemi Sasa ni kilimo Cha kujikimu Kwani tunawafanyabiashara wadogo wanaokuwa kuelekea kufanya biashara kubwa za kilimo ndio lengo la Serikali na ndio lengo la Mh.Rais.
“Maonesho haya ya kilimo biashara ni dhana ambayo Serikali imekuwa ikifanyiakazi Kwa sehemu kubwa Sana lakini haijaacha kushirikisha wadau wote katika mnyororo wa thamani wa Kilimo ilikuhakikisha tija kwenye uzalishaji inaongezeka na pia walaji wanapata uhakika wa chakula na lishe bora”
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa kilimo nchini TARI Dkt.Geofrey Mkamilo amesisitiza malengo ya Serikali kuelekea 2030 kuongeza tija katika kilimo ikiwemo kufikia uzalishaji unaondoa upungufu wa uagizaji wa chakula nje ya nchi.
Amesema kwamba Serikali kupitia mazao ya kimkakati imejipanga kuhakikisha uagizaji huo wa mazao unakwisha na nchi inajitosheleza Kwa chakula sanjari na kuzalisha mazao yenye lishe yanayohitajika katika soko ikiwemo usalama wa chakula na kuendana na mabadiliko ya tabianchi.
Nae mkulima Dausen Ayo Kijiji cha kitivu aliye shiriki Maonesho hayo Amesema kwamba wakulima wanakabiliana na changamoto mfano mwaka huu wamelima Kwa kufuata maelekezo ya utaalamu lakini Mahindi yakapekechwa kwenye mberewere na tumesumbuka Sana hivyo Serikali itusaidie Sana kuzalisha mbegu Bora zinazoendana na mabadiliko ya tabianchi.