………………
Na. Sixmund Begashe
Hifadhi ya Taifa Mikumi imekuwa kimbilio la Watalii wengi wa ndani na nje ya nchi, kutokana Matokeo chanya ya Filamu ya The Royal Tour, miundombinu rafiki inayowezesha ndege kubwa kutua na kuondoka kwa usalama pamoja na Barabara zinazopitika vizuri kwa Magari madogo na Makubwa.
Akizungumzia juu ya ongezeko kubwa la watalii, Mkuu wa Hifadhi hiyo, Kamishna Mwandamizi Msaidizi Ignance Gara, amesema ni kutokana na Mchango mkubwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Filamu ya The Royal Tour pamoja Mradi wa Kukuza na Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), unaoendelea kutekelezwa kwenye Hifadhi hiyo yenye vivutio lukuki nchini.
Naye Rubani wa ndege ya Flightlink Bw. Khalid Amarjit, amesema wanajisikia amani wanavyo ona maboresho makubwa katika Hifadhi hiyo, kwani kwao inawarahisishia kutua na kuruka kwa amani huku akiipongeza Serikali kwa hatua hinayoichukuwa ya kuboresha miundombinu na Kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo Kusini mwa Tanzania.
Akizungumza kwa furahaa kubwa baada ya kutua kwenye Hifadhi ya Mikumi, Mtalii kutoka nchini Israel Bi. Lee Gad, amesema baada ya Utalii visiwani Zanzibar ameshawishika kutembelea Hifadhi ya Mikumi ili kujionea Utajiri Mkubwa wa Wanyamapori na Mimea uliopo nchini kwani kwa muda mfupi utaweza kuona Simba, Chui, Tembo, Twigwa na wengineo.