Wanawake wanaogombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wametakiwa kujiamiani kuwa na uwezo wa kuongea hadharani pamoja na kuzijua sheria na taratibu zote za uchaguzi ili waweze kupata ushindi wa kishindo.
Rai hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 24,2019 na Mwanasheria kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania ‘TGNP Mtandao’ Theresia Sawaya wakati akifunga mafunzo ya uongozi kwa Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019 yaliyofanyika katika ukumbi wa BM Maganzo wilayani Kishapu.
Alisema mbali na kujiamani,wanawake hao wanatakiwa wajue sheria za uchaguzi,ilani za vyama vyao,kanuni na taratibu zote za uchaguzi.“Unapogombea lazima utambue Je? una sifa za kugombea,unazijua taratibu na mbinu za kampeni?,Je unaijua ratiba nzima ya uchaguzi?. Haya yote yatakusaidia kukuwezesha kupata ushindi’,alisema Sawaya..
Sawaya alitumia fursa hiyo kuiomba jamii kuwapa nafasi wanawake kuongoza akisema wanawake wanaweza kuongoza na wanazo sifa za uongozi hivyo ni wakati sasa jamii kubadilisha mitazamo hasi inayomgandamiza mwanamke.
Mafunzo hayo ya uongozi yaliyofanyika Oktoba 23,2019 hadi Oktoba 24,2019 yalilenga kuwajengea uwezo wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019 ili waweze kugombea na kushinda kwa kishindo.
Katika siku hizo mbili za mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania ‘TGNP Mtandao’,washiriki wamefundishwa kuhusu dhana za jinsia na namna zinavyotumika na athari zake katika masuala ya uongozi, namna ya kufanya kampeni kwenye uchaguzi,kupata rasilimali fedha,ulinzi na usalama wa wagombea pamoja na mikakati itayowawezesha kugombea na kushinda kwenye uchaguzi.
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia Sawaya akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya uongozi kwa Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019. Mafunzo hayo ya siku mbili (Oktoba 23,2019 hadi Oktoba 24,2019) yameandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania ‘TGNP Mtandao’ kwa lengo la kuwajengea uwezo,ujasiri,mbinu na mikakati ya kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi na kushinda. Picha zote na Kadama Malunde
Watia nia kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wakijikumbushia mambo mbalimbali waliyojifunza siku ya kwanza ya mafunzo hayo Oktoba 23,2019.
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa (katikati) akisisitiza jambo wakati washiriki wa mafunzo hayo wakijikumbushia mambo mbalimbali waliyojifunza siku ya kwanza ya mafunzo ya uongozi Oktoba 23,2019.
Mjumbe wa kituo cha taarifa na maarifa kata ya Ukenyenge,Angelina Nhiga ambaye ametia nia kugombea uongozi katika kitongoji cha Bulimba kijiji cha Bulimba kata ya Ukenyenge akielezea mambo aliyojifunza siku ya kwanza ya mafunzo ya uongozi ikiwa ni pamoja na kujiamini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati washiriki wakikumbushana masuala kadha wa kadha waliyojifunza siku ya kwanza ya mafunzo hayo.
Diwani wa Viti Maalum kata ya Bunambiyu Mhe. Hellena Baraza akielezea mbinu mbalimbali za kushinda katika uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutokata tamaa.
Mwenyekiti kituo cha taarifa na maarifa kata ya Maganzo Esther Kaheshi akielezea umuhimu wa kuwa jasiri katika uongozi.
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa ambaye pia ni mwezeshaji katika mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa akitoa mada kuhusu masuala ya uchaguzi.
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia Sawaya akitoa mada kuhusu usalama wa wagombea kwenye uchaguzi.
Wawezeshaji katika mafunzo ya uongozi Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Theresia Sawaya na Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao Eva Hawa (kulia) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya uongozi kwa Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019 wakifanya kazi ya kikundi.
Kazi ya vikundi ikiendelea.
Washiriki wa mafunzo wakiendelea na kazi ya kikundi.
Kazi ya vikundi inaendelea.
Kazi za vikundi zinaendelea.
Washiriki wa mafunzo ya uongozi kwa Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019 wakiwa katika picha ya pamoja.
Washiriki wa mafunzo ya uongozi wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde –