Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akizungumza mara baada ya kufungua Kongamano la Kisayansi kuhusu ugonjwa wa Sickle Cell lililofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Julai 12,2023.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akizindua jarida mahususi kwa ajili ya ugonjwa wa Sickle Cell mara baada ya kufungua Kongamano la Kisayansi kuhusu ugonjwa wa Sickle Cell lililofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Julai 12,2023.
………………………………
JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi bilioni tano katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kupandikiza uloto pamoja na kuhakikisha wagonjwa wa Sickle Cell wanapata matibabu kwa wakati.
Akizungumza leo tarehe 12/7/2023 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kongamano la Kisayansi la Sickle Cell, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, amesema kuwa Tanzania kila mwaka wanazaliwa wagonjwa wa Sickle Cell 11,000 hadi 14,000 .
Amesema kuwa idadi hiyo inaifanya Tanzania kushika nafasi ya tano kuwa na wagonjwa wengi wa Sickle Cell duniani, ikifatiwa na Nigeria pamoja na
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.
“Katika Kongamano la Kisayansi tunaonesha jinisi gani serikali ya Tanzania ikifanya jitihadi ya kuwatambua wagonjwa wa Sickle Cell ili waweze kupatiwa matibabu” amesema Pro. Nagu.
Amesema kuwa utambuzi wa ugonjwa Sickle Cell unafanywa katika hospital saba za kanda, mikoa pamoja na hospital ya Taifa ya Muhimbili.
“Serikali tayari imetoa muongozo wa matibabu na namna ya kutiba ugonjwa Sickle Cell ambao unakwenda kuwasaidia watoa huduma nini cha kufanya na wakati gani katika kutekeleza majukumu yao” amesema Prof. Nagu.
Prof. Nagu amesema kuwa ugonjwa wa Sickle Cell umeleta madhara kwa watoto kutokana wamekuwa wakiumwa mara kwa mara.
Hata hivyo amefafanua kuwa katika Kongamano la kisayansi kuhusu Sickle Cell limewakutanisha wataalam kutoka nchi mbalimbali dunia ikiwemo Bara la Afrika, Amerika, Ulaya pamoja na Asia.
Amesema kuwa kongamano lina maudhui mawili ambayo ni kuzindua jarida mahususi kwa ajili ya Sickle Cell pamoja na kujadili namna ya kupunguza tatizo la Sickle Cell ulimwenguni.
Sickle Cell ni ugonjwa wa kurithi ambao
ambao unaathiri vina saba (Ugonjwa wa Genetics).
Picha ya pamoja