Na Sophia Kingimal
Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) kimeibuka kuwa miongoni mwa vyuo vikuu vitatu vyenye ubora wa juu katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.
Akizungumzia ushindi huo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema uanishaji wa ubora wa vyuo ulianzishwa Kwa lengo la kushughulikia changamoto zinazokabili sekta ya elimu ya juu katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Afrika.
“Uanishaji wa ubora unazingatia nyanja za ufundishaji,matokeo na utafiti kwenye maeneo ya msingi.”amesema Kamuhabwa
Ameongeza kuwa uanishaji huo umezingatia maeneo matano ambayo ni rasilimali na Fedha,upatikajia wa elimu na usawa,ujuzi wa kufundisha,ushirikishwaji wanafunzi na matokeo katika Afrika.
Amesema mapema mwaka huu MUHAS iliainishwa kuwa katika nafasi ya kumi miongoni mwa vyuo vikuu Bora Afrika ambapo katika uanishaji huo uliofanywa na THE(TIME HIGHER EDUCATION) 2023 ambao katika uanishaji huo wa ubora MUHAS kiliibuka chuo kikuu Cha Tano Afrika na kuwa katika kundi la vyuo vilivyo katika nafasi ya 401 hadi 500 Duniani.
Aidha kamuhabwa ameongeza kuwa MUhas imeweza kupata mafanikio hayo kutokana utekelezaji wa shughuli zilizoainishwa kwenye mpango mkakati wa chuo hiko ambapo mpaka Sasa Wana programu za masomo 103 ambapo 18 Kati ya hizo ni za uzamili.
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo tafiti ubunifu na ushauri Profesa Bruno Sunguya amesema kuwa uwepo wa tafiti nyingi za kitaalam imesaidia chuo kufika katika hatua hiyo.
“Tumekuwa na tafiti nyingi zenye ubunifu hii ni moja ya matokeo mazuri ambapo mpaka Sasa chuo kimefanya tafiti ya magonjwa mbalimbali kutokana na mahitaji ya Dunia.”amesema Prof Sunguya.
Nae Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo taaluma profesa Emmanuel Balandya amesema chuo kinaendelea kukua kitaaluma huku likiwa na mkakati wa kufungua TAWI la chuo mkoani Kigoma.