Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imetoa wito Kwa wananchi kutoa taarifa za watu wanaofungasha dawa kiholela bila kufuata utaratibu uliowekwa.
Akitoa taarifa hiyo Leo Julai 9 kwenye maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Meneja Uhusiano na Elimu Kwa umma Gaudensia Simwanza amesema TMDA imeweka utaratibu wa kumlinda mtoa taarifa ili kuhakikisha taarifa za usamabazaji na upakiaji wa dawa ambao unaweza kuleta athari Kwa mtumiaji unadhibitiwa..
“Taarifa yako Moja tu inaweza kuokoa watanzania maelfu ya watu hivyo niwaombe mtoe taarifa mtalindwa lakini mtaokoa wengine.”amesema Simwanza
Amesema taarifa inavyopatikana inachakatwa na kutumwa kwenye mfumo wa ukusanyaji taarifa unaomilikiwa na shirika la Afya Duniani ambapo baada ya kuchakatwa itatoa taarifa na kujua tatizo la dawa husika na kulifanyia kazi.
Amesema Sayansi ya dawa ni endelevu hivyo hata dawa kama imesajjiliwa bado itakapoanza kutumika itaendelea kufuatiliwa.
“Taarifa zinapopatikana na huchakatwa na ndio maana Kuna wakati utasikia shirika la Afya Duniani limeifuta dawa Fulani hii ni kutokana na ufuatiliaji unaofanywa mara Kwa mara wakati dawa ikiwa ipo sokoni”amesema
Ameongeza kuwa dawa inaposajiliwa na kuingia sokoni ufuatiliaji unaanza mara moja ambapo kufuatilia kwake Kuna kuwa na njia mbili ikiwa ni ukaguzi lakini pia kuingia katika maduka kununua na kupeleka kwenye maabara.
“Tunanunua zile dawa na kuzipeleka maabara ili kujiridhisha dawa tuliyoisajili na kuingia sokoni je ipo hivyo au kuna mabadiliko hii imetusaidia kugundua dawa duni ambapo dawa duni sio bandia ila zinatokana na mabadiliko ya Hali ya hewa au wakati wa kufungashwa hazikufaungashwi vizuri. na ndio maana tunafuatlia Kwani lengo la TMDA ni kulinda Afya ya mwananchi”amesema Simwanza