Na. Ashrack Miraji
Serikali imelazimika kutumia Helkopta kutafuta makundi ya wanyama wakali na waharibufu Tembo waliozagaa katika vijiji 25 vya wilaya ya Same na kuwavisha vifaa maalum vya Mawasiliano kufuatilia mwenendo wao miongoni mwa njia za kudhibiti athari za mwingiliano wa shughuli za kibinadamu na Uhifadhi.
Zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mohammed Mchengera alilotoa hivi karibuni alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika wilaya hiyo ya Same ambapo aliagiza Mamlaka ya hifadhi za Taifa TANAPA kupeleka Helkopta katika Wilaya hiyo kusaidia zoezi la kuondoa makundi ya Tendo yaliyozagaa katika maeneo mbalimbali na kuwarejesha katika maeneo ya hifadhii.
Oparesheni hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Taasisi Nne zilizo chini ya wizara ya Maliasili na Utalii,Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Same na Wananchi wenyeji ambao wanasaidia kuainisha maeneo walipo Tembo.
Akizungumzia utekelezaji wa Oparesheni hiyo, Mkuu wa hifadhi ya Taifa Mkomazi, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Emmanuel Moirana amesema kwa siku ya kwanza jumla ya makundi matano ya Tembo yamerejeshwa hifadhini, mkakati uliopo ni kuendelea na zoezi hilo kuondoa changamoto ya mara kwa mara kuripotiwa makundi ya Tembo kuonekana maeneo ya Nje ya Hifadhi.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amepongeza jitihada hizo za Wizara uharaka wa kutekeleza ahadi ya kuondoa Tembo hao kwa kuongeza vitendeakazi na rasilimali watu, akisema huenda changamato ikapungua na wananchi kuweza kuendeea na shughuli za uzalishaji.
“Baada ya kupata taarifa za ukubwa wa tatizo Mhe.Waziri aliagiza TANAPA kuleta Helkopta ndani ya Siku mbili kusaidia katika Oparesheni ya kuwajeshesha Tembo kwenye maeneo ya hifadhi, kwakweli zoezi sio rahisi sana lakini tunamshukuru mungu zoezi limefanyika kwa ufanisi mkubwa na wananchi wameonekana kufurahia kuona serikali yao ni sikivu”.Alisema Kasilda Mgeni-Mkuu wa Wilaya ya Same.
Baadhi ya waazi wa Wilaya ya Same walioshiriki katika Oparesheni hiyo wamesema kuna idadi kubwa ya Tembo ambao wametoka kbisa kwenye maeneo ya hifadhi na kufanya makazi ya kudumu kwenye maeneo ya vijiji, hali ambayo imesababisha baadhi yao hasa wakulima mwaka huu kukosa kabisa mazao.
“Madhara ya watu kuuliwa na Tembo kwa hapa kitongoji cha Kabambuu hayajatokeani athari tu za mazao kuliwa na Tembo yaani kunawatu hawatavuna kabisa hata chembe ya Mahindi kupeleka nyumbani kwao hakuna na niwengi wameathirika”. Alisema Sallum Omary Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kavambuu kata ya Same Mjini.
Taarifa iliyowasilishwa na Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni kwa waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa alipofanya ziara Julai 5, 2023 zinaeleza kumekua na ongezeko la matukio ya Tembo kuvamia kwenye maeneo ya makazi mwaka hadi mwaka.
Taarifa hiyo imeeleza kwa wilaya ya Same mwaka 2014 Ekari 17 za mazao ziliharibiwa, 2015 Ekari 22.5, 2016 ekari 27, 2017 ekari 125, 2018 ekari 421.5, 2019 ekari 757.25 na kifo cha mtu mmoja, 2020 ekari 421.5, 2021 ekari 475.25 na vifo vya watu wawili, 2022 ekari 620.9 na vifo vya watu wawili, wengine wawili kujeruhiwa sambamba na Vifo kwa Mifofu mitano na mwaka 2023 hadi kufikia mwezi Juni Ekari 1,121.9 za mazao zimeharibiwa, Mtu mmoja ameuawa na na mwingine mmoja kureruhiwa.