Akizungumza na waandishi wa habari July 8 mara baada ya kutembelea Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amesema kuwa katika sekta ya misitu wamekuwa wakitoa elimu juu ya uhifadhi wa misitu na rasilimali zinazotokana na misitu kama mbegu pamoja na kujikita katika kutoa elimu kuhusiana na ufugaji nyuki pamoja na bidhaa zake.
“Kuna misitu ya asili pamoja na misitu ya kupandwa ambapo lengo la sekta ya misitu ni kuhakikisha wanaimarisha mifumo yote”amesema Silayo
Aidha Katika kuhakikisha nchi inapata bidhaa bora kutoka katika rasilimali Silayo amesema TFS inaimarisha mifumo ya Ikolojia nchini ili iweze kutoa hewa safi na maji na kuwa na makazi bora ya wanayama pori.
Prof. Silayo ameongeza kuwa TFS imepewa wajibu wa kuhakikisha kwamba Nchi inapata bidhaa bora hasa za mazao ya misitu ili iweze kutumika kwenye maendeleo ya taifa kuanzia bidhaa za ujenzi, Nishati zinazotokana na mimea.
Sambamba na haya prof Silayo anesema kuwa wanaendelea kuhamasisha wananchi kujihusisha na ufugaji nyuki, Uchakataji wa Mazao ya nyuki, kuboresha mnyororo mzima wa thamani pamoja na usafirishaji katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
“Tumepata masoko makubwa nje ya nchi, Sasa ni wajibu wa wadau wetu wa ndani wanaofanya biashara za kimataifa kuyakaribia masoko hayo na kufanya biashara ya kimataifa pamoja na kuiwezeaha nchi kupata fedha za kigen”ameongeza Prf SILAYO
Amesema kuwa ufugaji wa nyuki wanaupa msukumo mkubwa kwani kunamasoko ambayo yameshafanyiwa tathmini za ubora za mazao ya nyuki nchini na zinakidhi vigezo vya uuzaji kwenye masoko ya nje ya nchi.
Amesema TFS wakishirikiana na Serikali wanashirikiana katika upandaji miti ili kuongoa maeneo yaliyoharibika, kuonesha uwekezaji katika maeneo ya viwanda na ambapo hivi karibuni imeweza kuongeza kiwango cha uwekezaji wa ndani na usafirishaji zaidi mazao ya misitu kuliko ilivyokuwa awali,
amesema miaka mitano iliyopita wakuwa kubiq mita (Q³) elfu ishirini na tano kwenda nje ya nchi na kuingiza Q³
Aidha Prof. Silayo ametoa wito Kwa wadau mablimbali kutembelea banda lao ili waweze kupata elimu juu ya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali zinazosimamiwa na TFS.
Akizungumzia kuhusiana na uhifadhi wa Misitu amesema kuwa wameweza kutoa mafunzo wa vijana mbalimbali walipo katika maeneo yenye misitu ili waweze kutoa taarifa, kuzuia na kuzima majanga ya moto yanapotokea katika misutu hapa nchini.
Amesema pia serikali imewekeza katika katika teknolojia za kupambana na moto, pia kutumia teknolojia ya Satelaite ambayo inaona moto kabla haujasambaa na kushika kasi na kuweza kutoa taarifa kwa njia za kidijitali ambazo zinasaidia kwenda kuuzima mapema.