VIWANJA TANZANIA ni sehemu ya kampuni ya Prime Location Investments Ltd. Ni jina la biashara na idara inayojihusisha na utoaji wa huduma zinazohusiana na viwanja ikiwa ni pamoja na kuuza, kupima na ushauri.
Mbali na utoaji wa huduma za viwanja, kampuni hiyo inatoa huduma za Real Estate zikiwemo uuzaji na upangishaji wa majengo. Huduma zingine ni ushauri wa mambo yanayohusiana na Real Estate ikiwa ni pamoja na FURSA zilizopo na jinsi ya kuwekeza.
Tuna uzoefu wa zaidi ya miaka 14 katika utoaji wa huduma hizi na tumekuwa msaada mkubwa kwa wateja wetu wengi na wadau wengine.
Mnakaribishwa katika maonesho ya 47 ya biashara ya Kimataifa viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam katika banda la Ali Hassan Mwinyi ili kupata maelezo ya huduma zitolewazo na kampuni ya Viwanja Tanzania.
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu namna ya kynunua viwanja wakati walipotembelea katika banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Ivan Karugendo kutoka Kampuni ya Viwanja Tanzania akimpa maelezo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya Sabasaba.
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu namna ya kununua viwanja katika banda hilo.
Picha ya pamoja