Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa PETROLI PURA Bw. Charles Sangweni akizungumaa na waandishi wa habari Katika Banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Na Sophia Kingimali
Mamlaka ya udhibiti mkondo wa juu wa petroli (PURA) imetoa Rai Kwa wananchi kutembelea kwenye Banda lao lililopo kwenye viwanja vya maonyesho sabasaba ili kupata elimu kuhusu uchakataji wa mafuta ghafi na gesi iliyopo kwenye kina kirefu Cha bahari.
Akizungumza baada ya kutembelea Banda Hilo kwenye maonyesho ya 47 ya biashara Saba Saba Mkurugenzi Mkuu wa PURA Charles Sangweni amesema wao wanamalengo makubwa ya kuhakikisha wanafanya shughuli zao Kwa weledi
Amesema malengo yao ni kuhakikisha uzingatiaji wa vigezo vya kiafya,kiusalama na kimazingira katika shughuli za petroli ambapo wataimalisha ushiri wa wazawa na manunuzi ya bidhaa na huduma za wazawa katika tasnia ya petroli.
Aidha Sangweni ameongeza kuwa wanaendelea kutoa elimu Kwa umma kuhusu shughuli zinazofanyika katika uchakataji wa mafuta ghafi.
“Kwenye kuchimba kwenye mkondo wa juu unapata mafuta ghafi au gesi lakini pia unaweza kuchimba na usipate kitu”amesema,
Aidha Sangweni. ameongeza kuwa uchimbaji wa visima umekuwa na gharama kubwa ambapo kisima kimoja kinaghalimu pesa za kimarekani milioni 47 ambao visima 96 vilichibwa na ni visima 44 pekee ndio vimepata gesi na vingine kukosa kitu kabisa.
“Kuwekeza kwenye sekta hii ni kujitolea sana Kwani unakua huna uwakika kama ukichimba utapata kitu hivyo serikali imeingia mikataba na wawekezaji Kwa kujua wao wakifanikiwa sehemu ya wanachokipata kinabaki nchini”ameongeza Sangweni..
PURA inatekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 12 Cha Sheria ya petroli ya mwaka 2015 ambapo majukumu yake makubwa ni pamoja na kuishauri serikali juu ya mambo yanayohusu mkondo wa juu wa petroli.
Aidha PURA humshaauri wazir wa Nishati katika utoaji,usitishaji,ufutaji na uhuishaji wa leseni za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi.
Sangweni Ameongeza kuwa wanafanya kazi na serikali katika majadiliano ya mikataba ya ugawaji mapato PSA ambapo serikali huongia na wawekezaji ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali juu ya ugawaji wa vitalu.
Hata hivyo PURA husimamia miradi ya kusindika gesi asilia kuwa kimiminika ikiwa ni pamoja na kutoa leseni ya usafirishaji wa gesi hiyo.
Ameongeza kuwa dira kuu ya PURA ni kuwa mdhibiti wa kimataifa wa mkondo wa juu wa petroli anayesimamia shughuli na rasilimali za petrol nchini kwa maslahi ya kizazi Cha Sasa na kijacho.
“Ukiacha dira yetu lakini pia tuna adhimia kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli Kwa uwazi weledi na ufanisi ili kuchangia katika ustawi wa jamii na kiuchumi Kwa watanzania”amesema Sangweni