Afisa Uhusiano wa Jamii kutoka GGML, Doreen Dennis (wa pili kulia) akimuelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Magogo – Geita utakaokuwa uwanja wa nyumbani wa Klabu ya Geita Gold Football Club inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Mradi huu wa kijamii unafadhiliwa na AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited. Kulia ni Afisa Mwandamizi (Rasilimali Watu), Innocent Mushi.
Meneja Usalama kazini kutoka GGML, Isack Senya (wa pili kulia) akimpatia maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba namna Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited ilivyoweka rekodi ya kunyakua tuzo ya kimataifa kwenye masuala ya usalama kazini (Global Safety Awards).
………
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Felchesmi Mramba ametembelea banda la Maonesho la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam, na kushuhudia rekodi za kipekee zilizowekwa na kampuni hiyo kutoka mkoani Geita.
Katika maonesho hayo, GGML inajivunia kushiriki kwa mara nyingine tena huku ikiwa imenyakua tuzo ya Kimataifa ya masuala ya Usalama kazini (Global Safety Awards) pamoja na utekelezaji wa miradi kemkem ya inayoinufaisha jamii ya Watanzania.
Maonesho ya Saba Saba ambayo ni fursa kwa Tanzania kushuhudia matunda ya mafanikio yaliyotekelezwa katika nyanja mbalimbali pia yanatajwa kuwa fursa ya kusherehekea maendeleo ya sasa na kuangalia malengo ya taifa ya baadae.