NA DENIS MLOWE, IRINGA
WAFANYABIASHARA soko la Mitumba la Orofea Maghorofani mkoani Iringa wametoa wito kwa mbunge wa Iringa Mjini Jesca Msambatavangu na viongozi wa manispaa kuweza kuwaunganisha na taasisi na wahisani mbalimbali ili waweze kupata mikopo ya biashara.
Akisoma risala iliyoandaliwa na wafanyabiashara hao mbele ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Jesca Msambatavangu, Makamu Mwenyekiti wa Soko Hilo, Abuja Peter alisema kuwa viongozi wa serikali na chama kuwatembelea mara kwa mara kubaini changamoto wanazokabiliana nazo kuliko kusubiri matukio yatokee ndio wafike kuzitatua .
Aidha wafanyabiashara hao walizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo tangu wamehamia katika Soko hilo la Orofea Magorofani ni miundombinu ambayo si rafiki kwa wafanyabiashara hao.
Alisema kuwa wakati wa mvua vibanda vimekuwa vikiingiza maji hivyo vinatakiwa kuwekewa Cap na Gati Mabanda ili maji yaende sehemu moja kwani Hali iliyopo sasa ni mbaya.
“Mazingira Magumu maji kuingia ndani wakati wa mvua na aidha ukubwa wa vibanda uongezwe viwili kwa kimoja kwani ni vidogo sana na Eneo ambalo tunafanyia mnada hapa chini pasakafiwe kwani kipindi Cha mvua matope eneo nzima” Alisema
Peter aliongeza kuwa changamoto nyngn wanazokabiliana nayo Dampo lihamishwe lisogee mbele Zaidi kwasababu ya harufu kali na Moshi ambao unatokea eneo la hilo Dampo husababisha Upumuaji kuwa wa shida sana kwa madalali wakati wa kunadisha na wauzaji wa vibanda.
Alitoa wito kwa viongozi wa manispaa kuhakikisha kwamba Daladala zipite katika soko Hilo zikitokea maeneo ya ipogolo, zizi na maeneo mengine ili kushusha wateja na kupakia wateja wanaopata huduma katika soko hili kwa wakati.
Kwa Upande wake Mbunge wa Iringa Mjini,Jesca Msambatavangu akizungumza na wafanyabiashara hao wakati wa ziara ya kata kwa kata mara baada ya kusikiliza kero zao alisema kuwa changamoto hizo za soko Hilo zitashughulikiwa kwa uharaka zaidi.
Alisema kuwa suala la dampo lianze mara Moja na kuchangia kiasi Cha sh. 200,000 ili waliondoe lilopo sasa na kupelekwa eneo la mbali kutoendelea kuwaathiri wafanyabiashara.
Aliongeza kuwa changamoto ambazo wameziwasilisha zitafanyiwa kazi na uongozi wa manispaa ambazo ziko ndani ya uwezo wao.
Akizungumzia suala la bandari kwa wafanyabiashara hao Msambatavangu alisema kuwa Bandari ya Dar es Salaam haijauzwa na wanaoeneza habari hizo ni wazushi na waongo.
Alisema kilichofanyika ni Makubaliano ya Awali ya Uwekezaji kati ya Tanzania na Serikali ya Dubai yanayolenga kuimarisha ufanisi wa bandari hiyo kuliko ilivyo sasa.
“Hakuna bandari iliyouzwa, hakuna bandari itakayouzwa wala hakuna mpango wa kuuza bandari yoyote kwa sababu makubaliano ni kuboresha zaidi uzalishaji kwenye b,” alisema
Alisema wanabadilisha mwekezaji kwa Lengo la kupunguza gharama za bandari za sasa kwani kwa Sasa meli zinatumia muda mrefu Hali ambayo lazima mfumuko wa bei wa vitu utapanda
Msambatavangu alisema kuwa kitendo Cha meli kukaa muda mrefu bandarini gharama zake zinaongezeka hivyo hicho ndio kilichosababisha tuone mwekezaji yule anafaa kuweza kupunguza gharama za maisha katika kutoa huduma za bandari.
Alisema kuwa mkataba usio na muda ndio mzuri unavunjika wakati wowote pale ambapo mambo hayaendi vyema.