Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Agnes Kayola amewasilisha Nakala ya Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Malawi, Mheshimiwa Nancy Tembo, Jijini Lilongwe Malawi.
Tarehe 01 Julai, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu alimteua Balozi Kayola kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi.