Meneja Masoko na Masuala ya Biashara wa Benki ya TIB, Bw. Said Mkabakuli (kushoto), akitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo kwa wananchi, waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Tanzania.
Mchumi Mwandamizi, Idara ya Mipango ya Kitaifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Martha Luanda (kushoto), akitoa elimu kuhusu maaandalizi ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, kwa Bi. Sada Jamala Nassoro (kulia), aliyetembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Tanzania.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko ya Kodi -TOST, Bw. Robert Manyama (kushoto), akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana-CMSA, kutoka kwa Mchambuzi Mwandamizi wa masuala ya fedha, Bi. Mariam Mtunguja (wa pili kushoto), alipotembelea Taasisi hiyo iliyopo ndani ya Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Tanzania. Wapili kulia ni Afisa Uhusiano na Masoko, Bi. Stella Anastazi na wa kwanza kulia ni Afisa Utawala kutoka taasisi hiyo, Bi. Sharizadi Mrisho.
Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila (kushoto), akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu Soko la Bidhaa Tanzania, kutoka kwa Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya Masoko ya Bidhaa Tanzania -TMX, Bi. Saraphina Komba (katikati) baada ya kutembelea taasisi hiyo kwenye Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Tanzania. Kulia ni Afisa Mipango kutoka Taasisi hiyo Bi. Eva Msangi.
Maafisa kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha – IAA, Bw. Arnold Kavishe (katikati) na Bi. Bernadetha Inyasi (kulia), wakitoa elimu kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho, kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Tanzania.
Mchumi kutoka Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Edwin Kachenje (kulia), akielezea masuala mbalimbali yanayohusu ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Tanzania. Kulia ni Afisa Mipango kutoka taasisi hiyo Bi. Eva Msangi.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Dar es Salaam)