Makamu Mkuu Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka (wa kwanza kushoto) akiwasili leo tarehe 2/7/2023 katika Banda la Chuo Kikuu Mzumbe alipotembelea Banda Hilo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Kibiashara Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Makamu Mkuu Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Dkt. George Mofulu Mhadhiri na Mratibu wa Kozi fupi na Ushauri wa Kitaalam Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipotembelea katika Banda la Chuo Kikuu hicho katika Maonesho ya 47 ya Kibiashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Makamu Mkuu Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka akikabidhiwa zawadi na Dkt Lucy Massoi Mkurugenzi Kimtaifaji Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipotembelea katika Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 47 ya Kibiashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Dkt Lucy Massoi Mkurugenzi Kimtaifaji Chuo Kikuu Mzumbe kulia akiwa katika picha ya pamoja na Rose Joseph Mkuu wa Kitego cha Mawasiliano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye aliwahikuwa mtumishi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Makamu Mkuu Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka akipata maelezo kutoka kwa washiriki wa maonesho hayo kutoka Chuo Kikuu Mzumbe wakatia lipotembelea katika Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 47 ya Kibiashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Makamu Mkuu Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe baada ya kutembelea katika Banda la Chuo Kikuu hicho katika Maonesho ya 47 ya Kibiashara Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Rose Joseph Mkuu wa Kitego cha Mawasiliano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye aliwahi kuwa mtumishi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu hicho.
………………………………………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Wadau mbalimbali wa Maendeleo wametakiwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe ikiwemo kujenga hostel za wanafunzi wa Kike Ndaki ya Mbeya kwa kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.
Wito huo umetolewa na Makamu Mkuu Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Prof. Lughano Kusiluka leo tarehe 2/7/2023 wakati alipotembelea Banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Kibiashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Prof. Kusiluka amesema kuwa moja ya ajenda za Taifa ni kuhakikisha wanawake wanapata fursa ya kusoma katika mazingira rafiki.
Ametoa pongezi kwa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kufanya harambee ya ujenzi wa hostel za wanafunzi wa kike Ndaki ya Mbeya, huku akiahidi kuchangia shilingi milioni moja.
“Nitaendelea kutafuta fedha sehemu nyengine kwa ajili ya ujenzi wa hostel za wanafunzi ili kuhakikisha wanasoma katika mazingira rafiki” amesema Prof. Kusiluka.
Prof. Kusiluka amebainisha kuwa katika maonesho ya sabasaba ya mwaka huu Chuo Kikuu Mzumbe wamefanya vizuri kwani wamekuwa na banda bora.
“Nimetembelea mabanda mengi katika maonesho ya sabasaba lakini Chuo Kikuu Mzumbe wamekuwa na Banda bora” amesema Prof. Kusiluka.
Amesema kuwa katika kipindi Cha mwaka mmoja Chuo Kikuu Mzumbe wamepiga hatua kwani wameendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kufanya tafiti pamoja na kusaidia jamii kupitia programu mbalimbali.